The House of Favourite Newspapers

WIZ KID AZICHAPA KLABU

0
Msanii Wizkid.

MWANAMUZIKI kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’ anayetamba kwa sasa na Ngoma ya Medicine, amezichapa klabu na shabiki ambaye alikwenda kupiga naye picha bila ridhaa yake jambo ambalo Wizkid alionekana kutolifurahia.

 

Kwa mujibu wa gazeti moja nchini Nigeria, tukio hilo lilitokea juzikati katika Ukumbi wa Club 1089, Victoria Island, Lagos.

Wiz Kid.

 

AOMBA MSAMAHA

Hata hivyo muda mfupi baada ya tukio hilo, Wizkid aliomba msamaha kupitia kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram baada ya kutupia video akizungumza kwamba; “Watu wangu, mashabiki zangu, ndiyo rafiki zangu. Kilichotokea 1089, hakikuwa kitu kizuri kifutike kama hakikutokea.”

 

Mbali na kuomba msamaha Wizkid alizungumza pia juu ya ngoma yake mpya ya Medicine na kuwaomba mashabiki sapoti kwa kazi yake hiyo.

NA MWANDISHI WETU | SHOWBIZ | IJUMAA

 

Msami na Uwoya Wana Mazito, Shuhudia Mwenyewe

Leave A Reply