Lagos, Nigeria
MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria, Wiz Kid, leo ameionyesha saa yake ya almasi, kwenye mtandao wa Instragram.
Picha ya saa hiyo aina ya Rolex ilikwenda sambamba na maneno “Frosted!!! @josephfrostoflondon!!” aliyoyaandika kwenye mtandao huo.
Joseph Frost ni muuza vito mashuhuri jijini London, Uingereza, ambapo miongoni mwa wateja wake maarufu ni mcheza soka wa Togo Emmanuel Adebayor, na wanamasumbwi Amir Khan na David Haye.
Hivi majuzi mwanamnuziki huyo alifyatua ‘remix’ ya wimbo wake maarufu wa ‘Ojuelegba’ kwa kushirikiana na Skepta kwa mara ya kwanza jijini Lagos.


1 Comment