The House of Favourite Newspapers

Yanga: Usajili Wetu Ni Akili Kubwa, Ali Kamwe Atamba ‘Ni Mwendo wa Burudani’

0
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa usajili ambao wanafanya kwenye timu hiyo ni wa akili kubwa ukiwa na malengo ya kuongeza uimara kwenye timu hiyo.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Desemba 31, 2023 walifunga kwa utambulisho wa winga Augustino Okra raia wa Ghana ikiwa ni zawadi ya funga mwaka.

Ipo wazi kwamba Yanga ina kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara, inashiriki Kombe la Mapinduzi 2024, Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya makundi na Azam Sports Federation.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa wanatambua kwamba mashabiki wanapenda kupata burudani kutoka kwa wachezaji na kuona kitakachofanyika kwenye usajili.

“Akili kubwa inatumika kwenye kila idara namna ya usajili wa wachezaji pamoja na kuwatambulisha yote haya tunatoa somo kwa wengine na tunaamini watajifunza mengi zaidi kutoka kwetu.

“Benchi la ufundi linatambua kwamba ambacho kinahitajika ni matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza hilo lipo wazi ndio maana wachezaji wanajituma kutafuta matokeo mazuri kwenye mechi zetu zote,” alisema Kamwe.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka

Leave A Reply