MSANII wa muziki wa Bongo Fleva anayetamba na Ngoma ya Kata, Richard Sitta ‘Staric’ amesema kuwa kutokana na mapenzi yake makubwa kwenye tasnia ya muziki alijikuta akiingia kwenye mgogoro mkubwa na baba yake aliyekuwa akimtaka aende jeshini.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, tangu akiwa mdogo alikuwa na ndoto za kuwa mwanamuziki lakini alijikuta akiingia kwenye mgogoro huo na mzee wake baada ya kukataa kujiunga na jeshi licha ya baba yake kuwa mjeda na kukomalia kuwa mwanamuziki.
“Kama si kuimba basi ningekuwa mwanajeshi, kuna muda nikifikiria nahisi nilimkosea sana mzee wangu kutokana na kitendo cha kumgomea kwenda jeshini, lakini sikuwa na jinsi kwa kuwa mapenzi yangu ya dhati na ndoto zangu zilinisukuma nifikirie kuja kuwa msanii mkubwa ndani na nje ya Bongo, nashukuru ilifikia hatua mzee akanielewa msimamo wangu,” alisema.