ILIPOISHIA IJUMAA WIKIENDA:
Saa kumi juu ya alama, mama Pilima alipokea simu kwa namba asiyoijua, akajua ni baba Pili…
“Haloo…niambie baba Pili…wapi? Ooo…napajua…oke… we umeshafika? Haya nakuja sasa hivi mpenzi wangu…”
BANJUKA NAYO MWENYEWE…
Mama Pilima alichukua usafiri mpaka kwenye hoteli aliyoelekezwa na mwanaume huyo. Akaingia ndani mpaka chumbani bila kupotea ambapo alimkuta mwenyeji wake amejaa tele japo alikuwa hajavua nguo kwa sababu machale yalimcheza…
“Unajua nini…saa zile nakuita pale nilijishtukia, nikasema ni mwenyewe kweli yule…si unajua tena kuonana kwetu ni usiku? Siku ya kwanza usiku, jana usiku, leo ndiyo nimekuona mchana,” alisema mama Pilima huku akikaa kitandani…
“Kweli kabisa…hata mimi mwenyewe sikukujua haraka…” alisema mwanaume huyo akiwa anafunga mlango kwa funguo yeye mwenyewe ili kama kuna mchezo unataka kuchezwa na mwanamke huyo audhibiti mara moja.
“Nilikuona…ulikuwa unanitafuta kwanza kichwani…unajua kukutana baa nako ni shida! Halafu hata sauti yako si ile ya baa…nadhani ile inakuwa ya pombe…kama jana tumezichapa sana,” alisema mama Pilima akiwa anaachia tabasamu…
“Sawa…loo!”
Walikaa kimya kwa muda wakiangaliana kisha mama Pilima akaachia tabasamu la mahaba, akamsogelea mwanaume huyo, akambusu, akamkumbatia, wakakumbatiana. Wakaenda kitandani, puu!
“Baba Pili,” aliita mama Pilima kwa sauti ya chini sana…
“Niambie mpenzi wangu,” alisema mwanaume huyo.
Hapohapo mama Pilima akajiuliza tena ni kwa nini mwanaume huyo hataki kutumia jina la mama Pilima kama alivyozea siku mbili za nyuma?
“Si leo tu lakini?” aliuliza mama Pilima, akimaanisha kwamba, baada ya siku hiyo wasipeane raha tena!
“Sawa, leo tu. Lakini si itategemea?”
Walicheka wote, wakaanza kuhamasishana kwa kushikana sehemu mbalimbali za mwili.
Mara, simu ya mama Pilima iliita lakini ilionekana huyo mtu aliyepiga kama alibip! Kwa hiyo hakuiendekeza, akaendelea na raha zake kitandani.
Walifika mahali wakachojoana ili safari iendelee. Mama Pilima akawa analalamika kwamba ni mara yake ya kwanza kuchepuka…
“Yaani mi leo jamani…yaani sijui itakuaje? Yaani wewe,” alisemasema mama Pilima.
Kazi ikaanza, shughuli ikapamba moto, safari ikakolea, mechi ikachezwa kwenye uwanja binafsi.
Mama Pilima akajikuta akiachana na kulalamikia kuchepuka, akaanza kusikilizia uhodari wa mwanaume huyo na kuzianzisha zile kelele zenyewe sasa.
Ilikuwa fujo, balaa na hekaheka. Ilibidi mwanaume huyo kumziba kinywa mama Pilima ili kelele zake zisiwafaidishe wapangaji wa kwenye vyumba vingine.
Shughuli ilipomalizika, walitulia, wakawa wanahema kwa kasi huku wakipongezana wenyewe kwa wenyewe…
“Hivi baba Pili, tutaweza kweli?” alisema mama Pilima…
“Kuhusu nini?”
“Kwamba baada ya leo na iwe basi?”
“Mh! We unasemaje kwani?”
“Mh! Ngoja tuangalie maana naona umenipa kitu kigeni sana mwilini mwangu. Leo nimesikia kama nabembea kwenye kamba iliyo chini ya mtu mkubwa wenye kutoa kivuli na upepo mwanana toka pwani,” alisema mama Pilima huku akitoka kitandani kuifuata simu yake ambayo ilikazana kuita…
“Sijui atakuwa nani? Labda mume wangu,” alisema kwa sauti mwanamke huyo huku akiishika simu hiyo.
“Hee! Mbona sielewi,” alishtuka. Ni baada ya kuona kwenye skrini jina Baba Pili ambaye yeye aliamini yupo kitandani, akaipokea huku akimwangalia kwa wasiwasi mwanaume huyo kitandani…
“Haloo…”
“Haloo, mama Pilima, mzima?”
“Mi…mzima…hebu subiri na…nakupigia,” alisema mama Pilima na kukata simu, akarudi kitandani…
“Hebu niambie ukweli…wewe siyo baba Pili?” aliuliza mama Pilima huku akionekana kuwa na sura iliyojaa hofu…
“Ni kweli,” alisema mwanaume huyo.
“Imekuaje ukanidanganya sasa?”
“Sijakudanganya, ila wewe uliingia kichwakichwa kwangu. Mimi si baba Pili,” alisema mwanaume huyo kwa sauti yenye unyenyekevu wa hali ya juu.
Mama Pilima alichuruzisha machozi, akajiinamia. Akamwangalia mwanaume huyo kwa macho yaliyojaa aibu akiwaza…
“Sasa huyu si amenielewa kuwa mimi ni mwanamke malaya. Lakini ni kwa nini nilimfananisha na baba Pili?”
“Usiumie mpenzi…tunaweza kuendelea na uhusiano…mimi nimekukubali sana. Hata muda ule unaniita, niliamua kuendelea kusimama na kuongea na wewe kwa sababu nilikupenda ghafla palepale, nikaona nimepata bahati ya mtende kuota jangwani,” alisema mwanaume huyo.
Mama Pilima alimwangalia weee, lakini moyoni akakubali kwamba, ni mwanaume mzuri kwake na amemtendea haki. Ina maana akiamua kusema basi, halafu akaendelea na baba Pili atakuwa ameanza tabia ya kurukaruka…
“Kwani wewe kwa jina la mtoto wako yeyote yule unaitwa baba nani?” mama Pilima alimuuliza mwanaume huyo huku akimwangalia kwa macho yaliyojaa mahaba mazito…
“Naitwa baba P.”
Je, unajua nini kilitokea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, siku ya Jumatatu.
Nunua Gazeti la Amani kila Alhamisi usome zaidi machombezo ya Irene Mwamfupe Ndauka.
Hongera,stori zako taamu sana endelea kuburudisha