×

Waziri Alipokiri Kuwa Mchawi-31

Wakati natoka mle ofisini niligeuza uso wangu nikaitazama tena ile ofisi. Nilihisi kama nilikuwa naagana nayo. Huenda nilikuwa naitwa kufukuzwa kazi.
Nilishuka ngazi taratibu huku nikiwaza. Maafisa wa wizara yangu niliopishana nao kwenye ngazi pia walinishangaa kuniona hivyo. Nilikuwa kama mgonjwa. SASA ENDELEA…

Kama ninaitwa kufukuzwa kazi, nilijiambia, nijiandae pia kufunguliwa mashtaka ya kufanya vitendo vile vya uchawi nyumbani kwa waziri mkuu.Lakini mbali ya hilo niliendelea kujiambia, ningewezaje kukabiliana na aibu mbele ya mawaziri wenzangu na mbele ya Watanzania?

Nikajihisi kuchanganyikiwa kiasi cha kupata wazo kuwa nisiende tena kwa waziri mkuu bali nikimbie. Wazo hilo la kukimbia nililiona kama ufumbuzi wa kuniepusha kuaibika na kufunguliwa kesi.

Lakini wakati nashauriana na akili yangu likaja wazo lingine kuwa nisikimbie. Wazo hilo liliniambia nikikimbia nitaonekana mpumbavu na pia nitajidhihirisha kuwa nilikuwa waziri mchawi.

Kukazuka mabishano makali ndani ya moyo wangu. Uso wangu ukataharuki, nikaona mwili wote umenifumka jasho.
Sauti moja ilikuwa ikiniambia; ‘Kimbia’.
Sauti nyingine ikaniambia; ‘Usikimbie’.

Kadiri nilivyokuwa nashuka ngazi sauti hizo zilizidi kuchagiza.
“Kimbia…usikimbie…kimbia…usikimbie…”

Nilikuwa kama mtu niliyekuwa nimeanza kuchanganyikiwa. Bahati njema kilichokuwa moyoni mwangu nilikuwa nikikihisi mimi mwenyewe. Laiti zile sauti zingekuwa zikisikika nje nisingekuwa na tofauti yoyote na kichaa.

Mpaka namaliza kushuka ngazi bado sauti hizo zilikuwa zikiendelea kushindana.
“Kimbia…usikimbie…”

Ule upande uliotaka nisikimbie ulipata nguvu, nikaamua nisikimbie. Nikajipakia kwenye gari na kumwambia dereva wangu:
“Nipeleke ofisini kwa waziri mkuu.”
Wakati gari linaondoka nilijiambia:
“Potelea mbali litakalotokea nalitokee.”

Nilifika katika ofisi ya waziri mkuu dakika chache tu baadaye. Nilishindwa kumtazama waziri huyo usoni kwa aibu hasa nilipokumbuka vile vitendo nilivyovifanya nyumbani kwake usiku uliopita.
“Karibu kiti,” waziri mkuu akaniambia.
Nikakaa kwenye kiti mbele ya meza yake huku macho yangu nimeyaelekeza kwenye bendera ya taifa iliyokuwa pembeni mwa meza yake.

“Pole sana kwa matatizo yaliyokutokea,” waziri mkuu akaniambia.
“Matatizo yapi mheshimiwa?” nikamuuliza.
“Nilipata habari kuwa majambazi yaliiba gari lako jana usiku halafu gari hilo likakakamatwa na polisi.”

“Ni kweli,” nikamwambia na kuongeza:
“Gari langu liliibiwa jana usiku. Hii leo asubuhi ndiyo nilikabidhiwa na polisi.”
“Ilikuwaje?”

Nikamueleza mheshimiwa huyo kama nilivyoandikisha kule polisi.
“Pole sana. Nitamuagiza waziri wa mambo ya ndani ahakikishe kuwa doria zinaimarishwa usiku na mchana. Vitendo vya ujambazi hasa uporaji wa magari vilikuwa vimekwisha lakini sasa vinaanza kuibuka upya.”

“Ni kweli mheshimiwa. Lakini bado ninawasifu polisi kwa sababu wamefanikiwa kulipata gari langu hata kabla sijakwenda kuripoti polisi.”

“Mimi pia nilipata mkasa jana usiku,” waziri mkuu akanikatisha. “Kuna mtu aliingia nyumbani kwangu akaweka kinyesi chake mbele ya mlango wangu.”
Nikajifanya nashtuka.
“Huyo atakuwa kichaa!”

“Polisi wameniambia alikuwa yuko uchi wa mnyama na alitoweka kiajabuajabu.”
“Aliingiaje wakati kulikuwa na polisi kwenye geti?”

“Nimewaambia polisi wafanye uchunguzi halafu waniletee taarifa kamili. Nataka nimjue yule mtu na pia nijue ni kichaa kama ulivyosema au alikuwa mzima. Kama ni mtu mzima nataka nijue alikuwa na maana gani kwenda kuniwekea kimba kwenye mlango wangu.”

Wakati waziri mkuu akiniambia hivyo nilikuwa nimeuinamisha uso wangu chini. Moyoni mwangu nilikuwa najiuliza kama waziri huyo alikuwa hamjui kweli aliyefanya hivyo au alikwishajua kuwa ni mimi bali alikuwa ananitega.

“Mimi nafikiri anaweza kuwa ni kichaa. Mtu mzima na akili zake hawezi kufanya hivyo,” nikamwambia huku nikitazama pembeni.
“Kama ni kichaa aliingiaje kwenye geti mahali ambapo palikuwa na askari na alitoka vipi bila kuonekana?”

“Mimi nadhani hawa askari wanalala usiku.”
“Ndiyo nataka kupata taarifa yao ili niweze kuchukua hatua.”
Pakapita kimya kifupi kabla ya waziri huyo kuniambia:

Leave a Comment