×

Mazishi ya tajiri mtoto, Moshi yazizima

20160104004127
Marehemu, Joseph Frank Maole enzi za uhai wake.

Na Mwandishi Wetu
MJI wa Moshi ambao ni Makao Makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro, Jumamosi iliyopita uligubikwa na simanzi wakati wa mazishi ya marehemu, Joseph Frank Maole ‘Tajiri Mtoto’ (36) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Siku hiyo ya mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya nyumbani kwake, Magereza, mji wa Moshi ulipoa, watu wakiwa katika makundi, wengi wakiushangaa Mkoa wa 20160104004143

Waombolezaji wakiuzika mwili wa marehemu.

Kilimanjaro kwamba sasa unakuwa maarufu kwa mauaji ya wafanyabiashara wakubwa.
Agosti mwaka 2013, mfanyabiashara wa madini Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, Erasto Msuya aliuawa maeneo ya Boma Ng’ombe, wilayani Hai, Kilimanjaro kwa kupigwa risasi kumi kifuani.

Desemba 2014, mfanyabiashara maarufu wa Moshi, Augustino Mallya, yeye alijiua kwa kujipiga risasi mwenyewe akiwa nyumbani kwake Magereza Karanga katika Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro. Chanzo hakikujulikana.

20160104004151

…..Wakiweka mashada ya maua.

Novemba 2013, mfanyabiashara mwingine maarufu, Nickson Mushi, aliyekuwa mkazi wa Msasani Maili Sita wilayani Hai, Kilimanjaro, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kwa kumvamia nyumbani kwake muda mfupi baada ya kurejea kutoka katika shughuli zake na kumpora Sh. milioni 18 na simu mbili.

Marehemu Maole alipigwa risasi Desemba 30, mwaka jana, nyumbani kwake eneo la Magereza, Mtaa wa Katanini jirani na Barabara ya Kibosho akiwa anaingia ndani ya nyumba yake akitokea kwenye biashara zake.20160104004159

Kwa mujibu wa majirani, marehemu alipigwa risasi mbili, kiganjani na ya kifuani ambayo inaaminika kuwa, ndiyo iliyomtoa uhai wake.

Inadaiwa kuwa, wauaji hao walitokomea baada ya kutekeleza mauaji hayo na hakuna kitu chochote walichochukua jambo ambalo linaamsha hisia kwamba, huenda ni mauaji ya kisasi au wivu wa biashara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Ramadhan Mungi, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kwamba, watuhumiwa wa tukio hilo wanasakwa.

Leave a Comment