Na Mwandishi Wetu
Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Makame ‘Joanita’ amesema kuwa, filamu yake mpya ya Nitakufa Kwa Ajili Yako imemfanya atembee kifua mbele kutokana na ubora wake ila akatao rai kwa wadau kununua kopi orijino badala ya feki ili wasanii waweze kunufaika.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Joanita alisema kuwa filamu hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Hamadombe Distributor imepokelewa vizuri na akawataka wale wapenda filamu kutonunua filamu feki kwa kuwa kufanya hivyo watawafanya wasanii wasinufaike na kazi zao.
“Najisikia faraja sana kuona filamu yetu hii imepokelewa vizuri mtaani, kikubwa tunaomba sapoti kwa wapenda filamu kununua zile ambazo ni orijino badala ya feki, wakinunua feki, hatutalifaidi jasho letu na badala yake tutakufa maskini,” alisema Joanita.