×

Mh! Eti Gilla ajipanga kumpindua Tunda

MAYASA MARIWATA
TUMEINYAKA! Eti yule msanii wa filamu Bongo Glasnost Kalinga ‘Gilla’ amesema kuwa, miongoni mwa vitu vinavyomchoma kumoyo kwa sasa ni kapo ya Mbongo Fleva David Genzi ‘Young D’ na video queen Tunda Sebastian, kwa kuwa longi taimu alishawahi kujiachia kimalovee na mwanamuziki huyo.

Huku stori ikiwa mbichi kabisa na kudakwa na Ubuyu wa Town, Gilla alisema kuwa anaumia jinsi wawili hao walivyoshibana kwenye uhusiano wao na kujikuta akitamani kulifufua penzi lililokufa sababu kuna mambo madogo ambayo ndo’ yalisababisha wakakosana.

“Huwezi amini nimelimisi sana penzi la Young D, namlaani sana Tunda kunipora mwanaume wangu, nitafanya juu chini kuhakikisha nampindua huyo demu na kumrudisha Young D wangu,”alisema Gilla na kuweka nukta.

Leave a Comment