Asalam alaykum mashosti zangu popote pale mlipo, naamini mmemaliza vema Sikukuu ya Valentine ambayo najua kila mmoja alikuwa na shughuli ya kumuonesha mpenzi wake jinsi anavyojua malavidavi!
Lakini kuna jambo moja, kwa wapenzi wa kweli au walio katika ndoa, Valentine’s Day ni siku tu ya kuhamasisha mshikamano, lakini ukweli upendo na mapenzi hayasubiri siku maalum, bali kila siku kwani hayasubiri maadhimisho babu, muoneshe unampenda kila siku ashindwe yeye tu!
Baada ya kukukumbusha hayo, nataka sasa nikueleze kitu adimu ambacho wanawake wengi mnashindwa kukifanya, kisa eti ni aibu na kwa kukazia zaidi, wanadai eti si utamaduni wetu Waafrika.
Mimi Shangingi Mstaafu nakwambia siyo aibu kabisa ni lazima mwanamke ujiamini, mwambie mpenzi wako au mumeo, bwana mimi nataka ile kitu roho inapenda, mbona kawaida tu! Ukimuacha, shauri yako usijejikuta unadoda shoga!
Kwa nini nakwambia utadoda, unajua siku hizi mambo yamebadilika mashost zangu, kwanza hali ya hewa halafu ishu ya kusaka mahela, akina baba mara nyingi hujikuta wanachoka na kusahau jukumu la ndoa nyumbani. Siyo ikiwa hivyo ukadhani kwamba hakupendi au ana mwanamke mwingine, la hasha!
Anakupenda sana huyo, ila ana majukumu mengi, ili kuifanya ndoa yako iendelee ku-shine, anayetakiwa kuwa mstari wa mbele kumkumbusha wa ubani wako ni wewe mwenyewe.
Unaweza kukuta una hamu na mumeo, unahitaji mechi, unashindwa nini kumwambia laivu bwana, si mumeo? Basi kama wewe unamuonea aibu shauri yako, wenzako michepuko wakimhitaji wanamwambia laivu waonane maana wana hamu!
Utasikia mwanamke anatoka na kumueleza shost wake kuwa siku nyingi mume wake hajampa haki yake, hivi huyo mtu atakusaidia nini wakati anayepaswa kulijua hilo ni mumeo?
Mfungulie moyo wako, mueleze kuwa unamhitaji, kwanza kuna faida nyingi za kumueleza umpendae kuwa unamuhitaji.
Huongeza mapenzi zaidi na zaidi kwani kwa kufanya hivyo anajua wazi kuwa wewe si msaliti, humjengea kujiamini pia kwani ataona bila yeye wewe huwezi kuridhika na mambo mengi zaidi!