×

Oya masela…. hata kama umetoboa lakini unaboa!

Inakuwaje masela wangu wa ukwehe? Ndo kama hivo mazee nipo fiti yaani chuma kabisa, nimetokea hapa ubaoni kibabe kukisanua ama nene? Basi mzuksi kama vepe kanyaga twende chama langu.

Washkaji ishu za Simba na Yanga si ndo hivo zimeshakrosi? Sori kwa wanangu mlioluzi na bigi apu sana kwa masela wangu mliowini. Kama vepe tuendelee kufaiti laifu ili mwisho wa dei tuzimeki na kuweka heshima kitaa si ndo mpango mzima aisee jamaa?

Makachala wakati f’lani hivi naona kama machalii wanajitoa kitu cha fahamu na kufanya ishu ambazo zinazingua kinoma. Ngoja niwape listori moko la mwananetu ambaye amehaso ileile bati baada ya kutobo na kushika mabovu anadistabu machizi kwa fasi ya kitaani.

Kabla ya mambo kuwa levo, kaka mkubwa Jeifoo alikuwa na respekti ile mbaya kwa masela bati ametoboa juzikati na kuanza kuleta za kuleta kwa wakuu wa kitaa.

Unaambiwa jamaa anachili kitaa cha wajanja cha Sinza kwenye geto ambalo masela wana kijiwe chao kwa saidi ya dirishani. Sasa bana kinachofanya kitaa kinammaindi ni kwamba anachenji maduu hadi inakuwa siyo ishu aisee arifu.

Ilikuwa lasti wikiendi masela wanamaindi kushea maaidia na mtu mzima Mpeke. Basi bana, pipo tupo tunapiga mastori ya hapa na pale kuhusu ishu za kutumbuliwa majipu huku masela wakimaindi kitaani kama mkwanja umekata f’lani hivi.

Hapo ndo likaibuka stori la mwanangu mwenyewe mazee, unaambiwa jamaa anaingiza totozi geto kama hana akili nzuri. Wanangu kwa saa bee tulizochili kwa kijiwe kaka mkubwa alizamisha geto mizigo mitatu.

Mi nikaona niwazingue kidogo wana kwa kuwaambia kuwa inawezekana ni masista zake. Wakaniambia hakuna ishu kama hiyo kozi kila kinachohapeni machalii walikuwa wanapiga chabo kwa dirishani.

Ebana makachala kuingiza vichenchede geto haikuwa topiki bati zile kelele za kwichikwichi ndo ishu kozi wana walikuwa wanakula tu wepesi na kusikilizia mastimu.

Wana wanakuteli kuwa skendo za selaa kugonganisha magari kwa geto zimezoeleka na kwamba imefikia stepu hata ya kumsemea jamaa mbovu kwa uongozi wa kitaa na sasa pipo wanataka kuandamana ili mshkaji ahame skani kozi anawafundisha madogo ishu ambazo siyo kabisa arifu.

Eti kaka mkubwa anajiona mjanja na kuwaboa masela kozi ametoboa vihela mbuzi. Kama vipi wana wananiaminia, nikimtumbua hapa basi atakaa sawa kozi huu si ndo mtambo wa kuchenji tabia? Kama hataki basi apigwe tu.

Ebana wanangu tupo levo? Kama kwenye kitaa chako kuna kichwa kama msela wa kitaa bee dheni cheki na mimi kwa mahewa ili tumpange. Ama nene?

Leave a Comment