ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:
“Kwa ninavyomjua, yule hawezi kuamka tena mpaka asubuhi,” alisema Bony naye akienda chumbani, Aisha akamshika mkono…
“Please! Kama kweli hawezi kuamka tena, twende na mimi chumbani kwangu,” alisema Aisha…
SHUKA NAYO SASA…
“Huogopi baby?” Bony alimwambia Aisha…
“Niogope nini wakati umesema kwa unavyomjua, twende nikapate raha sweet.”
Bony alikubali, akaenda na Aisha chumbani akijua mkewe hawezi kuamka.
Kwa sababu na wao walikuwa chakari kwa pombe, ila walikuwa wakijiwezaweza, walipofika kitandani, walipanda kama mke na mume. Bony hakutaka kupoteza muda huku Aisha akijiweka sawasawa.
Mpambano ulianza, Aisha alimbana vilivyo shemeji yake. Wazo kwamba anasaliti hakuwa nalo. Alikuwa huru kama yupo na mume wake, Mudy!
Alikuwa akisema maneno yote, tena kwa sauti ya kujiachia mpaka ilifika mahali, Bony akawa anamfumba mdomo kwa kiganja.
Mchezo ulipokwisha, Bony alipumzika kidogo huku akibembelezwa na mikono ya Aisha…
“Ngoja niende sasa,” alisema Bony.
Aisha alimruhusu lakini eti alimsindikiza mpaka kwenye mlango wake, wakasimama hapo na kupeana madenda ya nguvu kisha Aisha akamalizia na mabusu…
“Mmm…waaaa…mwaaaa!”
“Kesho baby,” alisema Bony…
“Sawa honey,” alisema Aisha.
Alikuwa ndani ya kanga moja tu, akarudi zake chumbani kwake. Alijitupa kitandani na kuwaza…
“Ni kweli ninachokifanya si kizuri lakini sasa nitafanyaje?” alijiuliza…
“Kama kuiba acha niibe tu. Ikifika wakati natakiwa kuacha kuiba nitaacha. Kwa muda ambao mume wangu atakuwa nje ya nchi mimi nitaishije sasa?”
Kwa upande wake, Bony akiwa kitandani, alimuingiza kichwani Aisha…
“Lakini demu yuko bomba sana. Yaani yuko vizuri katika maeneo yote, kitandani lakini pia na jinsi alivyoumbika. Mh! Siwezi kumwacha Aisha, hata kama Mudy akirudi nitaendelea kuwa naye.”
***
Kulikucha, ni Jumapili kwa hiyo ndani ya nyumba hiyo hakuna aliyekuwa akienda kazini lakini pia hakuna aliyekuwa akienda kanisani ukimuondoa Aisha ambaye imani yake si ya Jumapili.
Aisha alikuwa jikoni akiandaa kifungua kinywa, Bony aliamka na kwenda kukaa sebuleni, Neema alikuwa bado anauchapa usingizi…
“Baby umeamkaje?” Aisha alifika sebuleni na kumsalimia Bony…
“Niko poa sweet, wewe vipi?”
“Nimeamka salama, naandaa chai, si utakunywa na mayai?”
“Yes! Kama mayai yapo vizuri zaidi,” alisema Bony. Aisha akamwangalia Bony kwa sekunde kadhaa kisha akaachia tabasamu zuri lenye mvuto, akaenda jikoni.
Wakati anakwenda, Bony alimkazia macho akameza mate ya tamaa maana Aisha asubuhi hiyo alivaa kanga moja tu…
“Daa! Mtoto ameumbwa huyu, Mudy alijua kuchagua bwana! Mke wangu Neema ni mzuri ndiyo, lakini kwa Aisha acha kabisa,” alisema moyoni Bony.
Na Aisha wakati anatembea kwenda jikoni alijua anaacha matatizo kwa Bony, kwa hiyo alizidisha mbwembwe wakati wa kutembea ili wowowo licheze kupitiliza kwa lengo la kumchanganya akili Bony. Alifanikiwa kwani Bony alisimama na kumfuata hukohuko jikoni…
“Sweetheart,” alimuita akiwa amemsogelea jirani kabisa eneo la begani…
“Niambie baby.”
“Unajua nakupenda sana? Yaani nakupenda mpaka basi. Mudy anafaidi sana,” alisema Bony huku kidevu chake kikiwa kimelalia bega moja la Aisha…
“Kwani wewe hufaidi baby? Mbona unafaidi pia. Hata mimi naona Neema anafaidi. Natamani ungekuwa wangu Bony, nadhani ningeinjio zaidi,” alisema Aisha kwa sauti ya chini ili hata kama Neema akitoka asisikie…
“Da! Sasa bahati mbaya kila mmoja kaangukia kwingine baby,” alisema Bony…
“Mimi ninachotaka kutoka kwako ni kiapo. Niapie kwamba huwezi kuniacha hata kama Mudy akirudi…”
“Sweet, mbona hata bila kiapo ndivyo ilivyo. Mimi sikuachi, labda libumbuluke,” alisema Bony.
Palepale, Aisha akamgeukia Bony, akamwangalia kwa macho yaliyolegea kupita kawaida. Hakuwa akitabasamu wala kucheka, akatoa ulimi, Bony akaupokea.
Wakaganda kwa muda huku kila mmoja akiwa ametumbukiza vidole kwenye masikio ya mwenzake hali iliyosababisha wasisikie.
Neema aliamka, akajua mumewe alishatoka chumbani. Akiwa na gauni lake la kulalia, akatoka. Kufika sebuleni hakumkuta mume wake, akaona aende jikoni ambapo aliamini atamkuta Aisha naye atamwambia alipo Bony…
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu ijayo.