ILIPOISHIA GAZETI LA RISASI JUMATANO:
Mama Rehema alirejea jikoni huku akiniacha mimi sebuleni, nimekaa kwenye kochi lingine.
Tulikutana macho na baba Rehema, akaachia tabasamu na mimi nikaachia la kwangu, tukakaziana macho, nikayaona ya kwake yanaanza kulegea na mimi nikayalegeza ya kwangu, nikamwona anasimama, ananifuata nilipokaa, akakaa pembeni yangu, akanikumbatia kweupee kabisa aka…
SASA TAMBAA NAYO MWENYEWE…
…akanisogelea zaidi, sasa nikaanza kuogopa kwamba huenda alikuwa anafanya makusudi tufumwe na mke wake…
“Baba Rehema, yaani mkeo yupo jikoni tu hapo halafu wewe unanifanyia hivi?”
“Niachie mimi Jamila.”
“Mh! Mimi naogopa bwana.”
“Basi twende chumbani kwako,” baba Rehema alisema jambo ambalo kwangu lilizidi kuwa baya…
“Baba Rehema itakuwa ngumu bwana.”
“Ugumu wake unatokana na nini Jamila?”
Hilo swali, baba Rehema aliniuliza kwa sauti ya juu kama vile jikoni hakuna mtu. Bahati nzuri mkewe alikuwa akikaangiza, kwa hiyo mafuta ya kupikia yalipokuwa yakidondokea kwenye kikaangio, yalitoa mlio wenye kumfanya mkaangaji asisikie lolote kutoka nje ya eneo la jiko…
“Mama akija ghafla, si jikoni ni hapo tu,” nilimwambia.
Baba Rehema alionekana kama mtu aliyeshtuka ghafla, akaenda kukaa kwenye kochi jingine, akaniangalia weee, akasimama kwenda chumbani kwake.
Mimi pia nikaamka kwenda chumbani kwangu, nilifikia kujitupa kitandani na kulala huku kichwani nikimfikiria baba Rehema kwamba, ni kwa nini alifikia hatua ile ya kuonesha waziwazi anaomba penzi pale sebuleni…
“Ina maana mimi nimemchetua sana kuliko hata mke wake mama Rehema au? Mbona kama amechanganyikiwa sana na mimi?!” nilijiuliza mwenyewe pale kitandani.
Labda nijielezee mimi nilivyoumbwa kama siyo kuumbika ili upate picha kwamba ni mtu wa aina gani! Je, nastahili kumzuzua mbaba kama baba Rehema ambaye ana sifa ya kuwa baba yangu mzazi?
Kiumbo, si mnene wala si mwembamba, niko kati. Sura yangu sasa… nina macho makubwa, wengine wanasema yana asili ya macho ya Kizungu, mimi sijui ya Kizungu yakoje!
Midomo minene, pua ya Kiafrika, nyusi juu ya macho ni nyingi sana kiasi kwamba wala sina sababu ya kupaka wanja na zipo kama zimechongwa. Nina alama nyeusi, wengine huita kidoti chini ya jicho la kulia.
Sijui, labda Mungu mwenyewe aliamua niwe hivi, mimi shingo yangu ni nene kiasi, lakini ina alama za duara. Inakuwa kama nimevaa vitu vya urembo.
Kifua ni flati sana, lakini kikibeba nido zilizochongoka kiasi kwamba, baadhi ya blauzi nikivaa nikatembea mitaani, wanaume wanagandisha macho yao kifuani tu.
Sijajaliwa tumbo kama la mama Rehema, labda kwa sababu bado msichana au kwa sababu yeye anapenda sana kula kila wakati kama mchwa.
Kiuno changu ni chembamba sana, tena sana! Na huwa najivunia hapo. Kwani nikivaa suruali au gauni la kubana huwa nawasumbua wale wanaume wenzake na baba Rehema.
Miguu yangu ni ya bia kwa asilimia mia moja bila kupunguza, sanasana unaweza kuongeza. Bia inajulikana ilivyo. Kwa kawaida mimi nikisema nivae skintaiti, wale watu husumbuka sana, wengine hushindwa kujizuia.
Ukijumlisha yote niliyoyasema sasa, watu wengi hukataa kwamba mimi si mfanyakazi wa kazi za ndani bali ni mtoto wa baba Rehema, yaani wana maana mimi ni dada yake Rehema…mh!
Basi, nilijikuta nimepitiwa na usingizi mzito kuja kushtuka, nilikuwa nashikwa mguu, nikafumbua macho. Baba Rehema alisimama mbele yangu akiniangalia kwa macho ya mlegezo…
“Baba, mama je?” nilimuuliza nikijikunja pale kitandani…
“Ameondoka.”
“Kwenda wapi?”
“Kwa mama Ashura.”
“Si atarudi?”
“Si sasa.”
“Mh! Baba unanidanganya wewe.”
“Kweli Jamila.”
Niliangalia saa yangu ndogo ya mkononi na kubaini kwamba, tangu nilipopitiwa na usingizi mpaka muda ule, nilikuwa nimetumia dakika kama hamsini na tano hivi.
Nilimuuliza baba Rehema sasa anachotaka ni nini mpaka aje chumbani kwangu, akasema…
“Acha maswali yako wewe.”
Ili kujiridhisha kwamba mama kweli hayupo, nilimwomba baba Rehema aniruhusu niende chooni lakini lengo ni kuona ukweli na uongo wa baba Rehema…
“Nakwenda chooni kwanza,” nilisema huku nikivaa kanga moja tu na kutoka.
Nilipotoka chooni, niliamini mama Rehema hayupo kwani ukimya ulikuwa mkubwa, nikasema moyoni huu ndiyo wakati wangu na mimi na baba Rehema. Nikarudi chumbani, nikafunga mlango maana baba Rehema alishatangulia kitandani…
“We Jamila.”
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo