×

Wasomaji wengine kunufaika tena droo ya 3

BAADA ya kufanyika kwa kishindo kwa droo ya kwanza na ya pili, wasomaji wengi wamejiandaa kwa wingi kunyakua zawadi nono katika droo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na kampuni inayochapisha Magazeti ya michezo ya Championi pamoja na Magazeti Pendwa ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Risasi na Ijumaa Wikienda, Global Publishers.

Akizungumza na Uwazi, Juma Hassan mkazi wa Mabibo, Dar alisema kuwa amekuwa mshiriki wa bahati nasibu kwa muda mrefu na wala hajakata tamaa kwani anaamini zawadi ya nyumba ni yake.

“Ujue ukishasikia neno bahati nasibu, siyo kitu cha kuacha kabisa. Nimekuwa nikishuhudia ndugu na majirani zangu wakibahatika mara kwa mara na bahati nasibu hizi hivyo nawasihi wengine wanunue magazeti haya ya Global kwa wingi kama nifanyavyo kisha wajaze kuponi na kutuma. Wanatoa zawadi nyingi na tumeletewa hadi nyumba,” alisema Juma.
Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema kuwa droo hiyo ya tatu inayosubiriwa kwa hamu na wasomaji wa magazeti hayo inatarajiwa kufanyika Machi 30, mwaka huu katika Viwanja vya Manzese-Bakhresa jijini Dar ambapo washindi watapata zawadi nono.

“Kila mfuatiliaji wa magazeti ya Global Publishers anatambua zawadi zinazotolewa kila droo ikifanyika. Droo ya kwanza tulimpata mshindi wa zawadi kubwa ya TV Flat Screen pamoja na King’amuzi cha Ting, Happyness Haule na waliobakia wote walipata zawadi kabambe kama vile seti ya vyombo vya jikoni, simu za kisasa, ving’amuzi vya Ting na nyingine nyingi.

“Katika droo ya pili pia tulishuhudia kwa mshindi kutoka Kibaha, Pwani ambaye ni Lucy Swai aliyejinyakulia zawadi ya Pikipiki ya Skymark huku zawadi nyingine zikitolewa. Kinachotakiwa ni kununua magazeti yanayochapishwa na Global Publishers kisha kujaza kuponi na kuituma kwa mawakala ama ofisini kwetu moja kwa moja,” alisema Mkanda.

Katika droo kubwa, mshindi atazawadia nyumba ya kisasa iliyopo Salasala-Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ikiwa na samani za ndani. Katika shindano hili watu walio chini ya umri wa miaka 18, ndugu wa wafanyakazi wa Global Publishers hawaruhusiwi kushiriki.

Leave a Comment