Hamadombe Band.
Na Mwandishi Wetu
Bendi ya Hamadombe sasa imebaki na vijana sita baada ya wawili kutupiwa virago hivi karibuni lakini imetamba kuendelea kutoa burudani bab’ kubwa katika shoo yao watakayofanya Jumapili hii ya Pasaka ndani ya Ukumbi wa New Vision Pub uliopo Ungindoni, Kigamboni jijini Dar.
Kiongozi wa bandi hiyo, Chudo Bright aliitonya safu hii kuwa, baada ya mchujo huo wamezidi kujiimarisha na sasa wamedhamiria kwamba kila wanapofanya shoo waache historia.
“Vijana wawili wameondolewa kwenye bendi kutokana na utovu wa nidhamu, sasa tumebaki vijana wa kazi tu, madansa wako vizuri kutoa burudani ya kipekee na waimbaji nao ni full mzuka, anayetaka kujua tumenogaje aje Jumapili pale New Vision Pub, hatutaremba, itakuwa ni burudani mwanzo mwisho,” alisema Chudo Bright.
Aliongeza kuwa, mbali na shoo hiyo kutakuwepo na sapraizi za kumwaga hivyo watu waje kwa wingi kusherehekea Pasaka na bendi hiyo ambayo imejipatia umaarufu mkubwa Bongo.