×

Msanii Bongo Muvi anusurika ‘kuuzwa’ Nigeria

Msanii wa Filamu Bongo, Edna John anayeishi Sweden amenusurika kupelekwa nchini Nigeria na wajanja kufanya biashara ya kuuza mwili.

Akizungumza na Showbiz Xtra kwa njia ya simu, Edna anayebamba na Filamu ya The Virgin alisema kuwa awali alikuwa akiwasiliana na kijana raia wa Nigeria aliyehitaji kuunganishwa na msanii Mercy Johnson anayebamba kwenye filamu Nollywood, lakini akaenda kinyume kwa lengo la kutaka kumpeleka kumuuza na siyo kuonana na msanii huyo.

“Tuliwasiliana na huyo kijana vizuri, cha ajabu akaanza kunibadilishia maneno akinikazania kujiingiza katika filamu za ngono na kwamba zinalipa na hapo ukawa mwanzo na mwisho wa kuwas-iliana naye. Nawasihi sana wasanii wenzangu wawe makini,” alisema Edna.

Leave a Comment