×

Unavyoweza kutunza kucha zako zisipate fangasi

Wiki hii kwenye urembo tutaongelea utunzaji wa kucha ili zisishambuliwe na fangasi ambao mara nyingi huwapata sana akinadada hasa wanaobandika kucha.

Wengi utawasikia wakisema ni mdudu bila kujua kuwa huenda wameshambuliwa na fangasi. Sasa ufanyeje ili kuziepusha kucha zako na fangasi?
Limao na mafuta ya mzaituni
Tiba na ulinzi tosha utaupata huku kwenye limao na mafuta ya mzaituni. Chukua kiasi kidogo cha maji ya limao, changanya na mafuta ya mzaituni, acha kwa muda wa dakika 30 kisha osha kucha zako.

Ukimaliza zifute kisha paka mafuta ya mzaituni halafu fanya kama unazimasaji. Lakini pia unaweza kutumia limao tu kusugua kucha zako mara kwa mara ili kuzipa ulinzi.
Mafuta ya chungwa
Nikisema mafuta yatokanayo na chungwa mtu hawezi kuamini lakini yapo na ni mafuta mazuri kwa ulinzi wa kucha zako.
Kila mara hasa ukiona dalili mbaya kwenye kucha zako hakikisha unapaka juu na ndani ya kucha sehemu kucha inapoanzia kukua, acha kwa muda wa dakika 30 kisha osha.
Kama una tatizo tayari tumia mara mbili mpaka tatu kwa siku.

Leave a Comment