×

Wacheza Pool Wakaidi Agizo la Magufuli

Stori: Richard Bukos

AGIZO la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kupiga marufuku mchezo wa pool table muda wa kazi limeonekana kupingwa na wapenzi wa mchezo huo.

Baada ya agizo hilo kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ya (OFM) Kilifanya doria sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam maeneo ya Sinza Magomeni, Kinondoni, Mabibo, Ubungo, Buguruni na sehemu nyingine ambapo wapenzi wa mchezo huo walionekana wakiendelea kujibweda na mchezo huo muda wa kazi. Miongoni mwa baa walizokutwa wapenzi wa mchezo huo wakiendelea kukaidi agizo hilo ni Soccer City iliyopo Sinza jijini jijini.

Licha ya wapenzi wa mchezo wa pool kuonekana kukaidi agizo hilo ambalo lengo la Rais Magufuli lilikuwa ni kuwasisitiza Watanzania kutumia muda mwingi kufanya kazi ikiwemo biashara ndogondogo, OFM ilipofika eneo la Shekilango pembezoni mwa Baa ya Jambo ilikuta kundi la wanaume zaidi ya 15 wakiwa wamezunguka wakicheza drafti.Miongoni mwa waliozunguka kuangalia mchezo huo na wengine kusubiri zamu zao za kucheza ni wafanyabiashara ndogondogo ‘Wamachinga’, mafundi gereji, madereva wa bodaboda na wengineo.

OFM ilizungumza na baadhi ya vijana walionaswa wakicheza pool ambapo kijana mmoja aliyekataa kutaja jina lake na kusema yeye ni dereva wa bodaboda anayefanya kazi yake usiku kucha hivyo haoni sababu ya kutocheza pool muda huo kwa kuwa yeye ndiyo amepata nafasi ya kupumzika.

Kijana mwingine anayefanya kazi ya kuuza kahawa alisema kama itaanza kamatakamata basi waangalie aina ya kazi ya mtu waliyemkamata vinginevyo watatuonea sisi ambao mchana ndiyo muda wetu wa kupumzika usiku kazi tu.

Leave a Comment