Oya masela inakuwa nini aisee arifu? Mambo kwa saidi ni mpango mzima. Hakuna kuremba si unajua tauni masti utumie akili na kileji manguvu?
Wanangu wenyewe vipi michongo huku mbona naona makachaa mnasongamana tu kidandara kwenye maishu ya kubeti? Siyo mpango mazee ni bora kutumia nguvu kupiga mkwanja kuliko kusikilizia ishu ya kubahatisha washkaji zangu. Au ndo mmeamua liserereke? Utajaza aloni kozi laifu linahitaji kichwa kuamua moko ama kusuka au kupiga para.
Huku na huku nipo kwenye mingo kitaa cha Kino, mtu mzima napiga mbishe za kusaka mabovu dei na naiti kama vepe tutalala kitu cha uzeeni. Si ndo nikashea aidia na mshua ambaye anaonekana kula chumvi kilo zake kadhaa!
Kwanza ni truu laifu limechenji so lazima mtu ukaze kozi wana kibao wanasizi kitaa wakila tu wepesi na kuwasarendea mawaifu wa washua ili wawatoe upepo. Si unanyaka zile za akina marioo? Siku hizi washkaji kibao wanamaindisha kulelewa bila kujua kuna watu walihaso kuzichanga ndo maana hao mawaifu wana mauwezo. Eti kigezo ni kwamba wao wana damu changa za kuwakimbiza mamanzi wa wana!
Basi bana, mshua akaona isiwe kitu. Akaniteli kuwa yeye alimeri mtoto mmoko mkare hatare ambaye alikuwa gumzo kinoma enzi hiyo kitaa cha Kino-Shamba. Anakuteli kuwa mbebiz alikuwa nachuro kala kabisa yaani chokleti.
Kweli laifu likawa bomba kinoma kozi mshua alikuwa anazimeki kwenye gavamenti hadi akaangusha bonge la mjengo kitaa hiyo. Wani dei si akagundua kuwa kumbe maiwaifu wake alikuwa anachiti na hausiboi wao kiasi kwamba ikafika steji akamtia ndimu na kumtimua.
Ebana mshua anaweka pleini kwamba aliamua kama mbwaimbwai tu bora akaozee kwa fasi ya Segerea watoto wa tauni wanaita Segedansi.
Mazee katika situwesheni ambayo hadi tumoro hajui nini kilihapeni akamwekea maiwaifu sumu kwenye msosi bati kilichomsapraizi kumbe ule msosi hakugonga mazeri wa makidi wake alimpelekea yule hausiboi ambaye baada ya kugonga akadedi bana.
Dah! Ulikuwa msala mmoko denja ileile bati mshua alichomoka kozi hakukuwa na maushaidi ya dairekti. Pamoko na hayo bati chama langu anajuta hadi tumoro.
Mmenisoma wana? Kama vipi potezea ishu za Kitonga dheni dili na haso zako ipo dei utachomoka tu jembe langu.
Sii yuu neksti wiki!