MSANII wa kitambo kunako Bongo Muvi, Latifa Moto ‘Tifa’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutwangwa talaka na mumewe aliyejulikana kwa jina moja la Michael.
Chanzo makini ambacho ni rafiki wa Tifa kilisema kuwa, Michael alikuwa mume wa ndoa na Tifa na siku moja alimuaga kuwa anakwenda Dodoma kikazi kumbe alikuwa akienda kuoa mwanamke mwingine.
“Watu wa karibu na Michael walimtonya Tifa kuwa mumewe huyo ameenda kuoa hivyo alivyorejea nyumbani msanii huyo alikuwa kama mbogo na kuamua kudai talaka.
Baada ya kupata madai haya, Amani lilimtafuta msanii huyo ambapo alikiri kuwa ni kweli aliachwa;
“Sipendi kuongelea sana hili lakini ni kweli nimepewa talaka, namshukuru Mungu naendelea na maisha yangu ya kila siku,” alisema Latifa kwa ufupi na kukata simu.
Baada ya kuzungumza na Tifa, Amani lilimpigia simu Michael ambapo alisema kuwa mtalaka wake huyo anatafuta kiki;
“Sitaki tena kumuongelea huyo mwanamke kwanza naona kama anatafuta kiki, yeye si aliomba talaka nimempa sasa nini anataka tena kwangu, ujue yeye ana mwanaume mwingine huko Tanga sasa ya nini kuendelea kupeana stress?” alisema Michael.