×

Kadja ageuka mwalimu wa GYM

Stori: MAYASA MARIWATA
MWANADADA anayefanya poa kwenye gemu la muziki Bongo, Khadija Maige ‘Kadja Nito’ baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu hatimaye amepata dili la kufundisha kwenye Gym iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.

Msanii huyo alifumwa na paparazi wetu kwenye gym hiyo ya Power on Fitness akifundisha wanafunzi wengine na kusema kuwa, kwa sasa muda mwingi anaumaliza hapo akiwa kama mwalimu na analipwa vizuri.

“Naamini wasanii wengi hawajafikia kiwango changu sababu kuna wengi nawafundisha. Kwa jinsi nilivyo hawa jamnaa wakaona bora wanipe hili dili. Isitoshe hata malipo yake ni mazuri, kuna siku nashinda hapa kuanzia asubuhi hadi saa nane mchana, kisha narudi saa 11 hadi saa 2 usiku, labda nipate dharura,” alisema Kadja.

Leave a Comment