.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Vipindi wa EATV, Bi. Lydia Igarabuza, mshiriki wa tamthiliya hiyo, Dayana William ‘Princess’ na Cojack Chilo ‘Shaka Zulu’.
Mmoja wa washiriki wa tamthiliya hiyo, Mrisho Salehe Zimbwe ‘Carlos’ akizungumza jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wasanii na wanahabari waliokuwa wamefika kwenye hafala hiyo.
Baadhi ya washiriki wa tamthiliya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.
KITUO cha televisheni cha EATV cha jijini Dar es Salaam kimetangaza kwamba kitaanza kurusha tamthilia kali inayokwenda kwa jina la ‘Siri za Familia’ kwa lengo la kuwapa watazamaji fursa ya kupata uhalisia wa maisha.
Tamthiliya hiyo itaanza kurushwa Aprili 25 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Vipindi vya EATV Bi. Lidya Igarabuza, jana alisema EATV imekubali kurusha tamthilia hiyo kwa lengo la kuinua vipaji vya nyumbani ikizingatiwa kwamba lengo kubwa la EATV ni kuonyesha vipindi vingi vinavyozalishwa kwa maudhui ya hapa nchini yanayoigusa jamii moja kwa moja.
Kwa upande wa wahusika katika tamthilia hiyo wahusika yaani waigizaji (characters) waliishukuru EATV kwa kukubali kuonyesha watu kazi zao na kwamba kwa kufanya hivyo kunatoa fursa kwao kuonesha vipaji vyao na kutoa ujumbe wenye maadili ya Kitanzania.
“Tamthilia hii itaonyeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu mfulilizo kila siku ya Jumatatu hadi Alhamisi saa 12:30 jioni hadi saa moja 7:00 jioni,” Bi. Lidya Igarabuza alisema.
Baadhi ya wahusika hao ambao wameipika tamthilia hiyo ni pamoja na Dayana William (Princess) ambapo kwenye tamthilia ataonekana kama binti ambaye akiona mtu mwenye pesa macho yote yanaelekea huko na atakuwa funzo kwa kinadada kutokana na uhalisia atakaouonesha.
Kojak Chilo (Shaka Zulu) ataigiza kama baba wa familia ambaye ni makini katika kujenga familia na kuonesha ukomavu katika utendaji wa kazi za familia.
Mrisho Salehe Zimbwe (Carlos) ndiye mhusika mkuu katika tamthilia hii ambaye ataonyesha namna siri za familia zinavyokuwa katika jamii na ndiye ataunganisha matukio mbalimbali.
Abdul Thomson ataigiza kama tajiri, ambapo Jacklin Gabriel ataigiza kama mwanamke jeuri ambaye ni mgomvi na ana msimamo katika mambo yake.
Aidha watazamaji wote wameombwa kuitazama tamthilia hiyo na ambao watakosa muda watatazama marudio ambayo yatatangazwa na kituo hicho kwa lengo la kupata ujumbe mahsusi uliopo kwenye tamthilia hii.
NA DENIS MTIMA/GPL
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, DOWNLOAD NA INSTALL APP HII ILIYOPO KWENYE PLAY STORE YAKO==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

