Na Mwandishi wetu
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya uigizaji Bongo, Fatuma Makame ‘Joanita’ ameeleza kuwa Video Queen Gift Stanford ‘Gigy’ na Tiko Hassan ambao wanatarajia kufanya kazi pamoja kwenye filamu iitwayo Mtoto wa Kijakazi hawawezi kufua dafu kwake kwani yeye ni mzoefu.
Video Queen Gift Stanford ‘Gigy’
Joanita aliyasema hayo na kuongeza kuwa mastaa hao ni ‘cha mtoto’ kwake baada ya Gigy kuposti kwenye mitandao kuwa, kwenye filamu anayo-tarajia kuicheza na Tiko pamoja na Joanita, atawafunika kwani anajua kizazi cha sasa kinataka nini.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Gigy aliandika: “Nimekula shavu la kucheza filamu mpya ya Kampuni ya Hamadombe Distributor iitwayo Mtoto wa Kijakazi’, Joanita, Tiko wataomba poo kwa mautundu na maubunifu yangu.”
