Kama kawa, kama dawa wiki hii kwenye safu yetu hii tunaye msanii wa filamu Bongo anayefahamika kwa jina la Dina lakini jina lake kamili ni Nasra Mohammed.
Mwandishi Wetu Imelda Mtema alimbananisha kwa maswali 10, akayajibu kwa ufasaha kama ifuatavyo;
Ijumaa: Mambo vipi Dina, nashangazwa sana na urefu wa nywele zako, ni urembo tu au zina kazi nyingine?
Dina: (kicheko) Yaani kwanza unapokuwa na nywele ndefu kama hivi ni kivutio kikubwa kwa mpenzi wako, kama hujui basi nikujuze kwamba hii ni silaha ya faragha. Baby wangu anapozishika wote tunakuwa hoi, upo?
Ijumaa: Unafikiri nywele tu zinatosha kumchanganya mpenzi wako faragha?
Dina: Kuna mambo mengine lakini hiyo ni moja ya chachandu, silaha zingine zipo.
Ijumaa: Hivi umeolewa,una mpenzi au mchumba?
Dina: Kwa kifupi nina mtu wangu, ananipenda na mimi nampenda ila ndoa bado.
Ijumaa: Unadhani kitu gani kilichomvutia huyo laazizi wako kwako?
Dina: Mwenyewe anasema umbo langu, kama unavyoona nina kiumbo f’lani ‘amazing’, so linapokuja suala la kukukuruka mbona ni balaa!
Ijumaa: Ni nguo zipi unapendelea kuvaa unapokuwa faragha na mpenzi wako?
Dina: Mara nyingi napenda kujifunga mtandio tu, kwa nini nijizibezibe mtoto wa kike mbele ya baby wangu?
Ijumaa: Ni chakula gani ambacho unapenda kula pamoja na mpenzi wako?
Dina: Ninapokuwa na mpenzi wangu Strawberry ni muhimu, tunaweza kula siku nzima. Pia najisikia raha kunywa naye juisi ya madafu.
Ijumaa: Ulishawahi kumfumania mpenzi wako?
Dina: Bado na siku zote namuomba Mungu isije kutokea maana nahisi nitakufa kwa presha.
Ijumaa: Kwa mfano unagundua mpenzi wako ana kifaa kingine tena bomba kuliko wewe, utafanyaje?
Dina: Wala sitapagawa, nitahisi kuna sehemu nakosea hivyo nitaongeza mautundu.
Ijumaa: Mbali na uigizaji unafanya kazi gani, au wewe ni wale wanaotegemea bwana kwa kila kitu?
Dina: Mimi ni mjasiriamali mdogo, nafanya biashara zangu zinazonipatia kipato.
Ijumaa: Mpe maneno matamu mpenzi wako kupitia safu hii.
Dina: Nakupenda sana, yanasemwa mengi lakini wewe unabaki kuwa mtu muhimu kwenye maisha yangu, sitakusaliti, nitakuheshimu na kukupa kila unachotaka.
