MKALI wa nyimbo za Taarab, Aisha Vuvuzela anatarajiwa kutambulishwa rasmi Jumapili hii (Mei Mosi) ndani ya Ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar.
Akizungumza na Showbiz mtaribu wa shoo hiyo, Seif Magwallu ‘Shiboli’ alisema kuwa mbali na kumtambulisha Aisha, watamtambulisha pia mkali mwingine Zubeda Mlamali.
“Mashabiki wa Jahazi hii ni fursa kwenu, kwa mara ya kwanza Aisha Vuvuzela pamoja na Zebeda watapanda jukwaa moja na Jahazi kupiga shoo ambayo haijawahi kutokea,” alisema Shiboli.