×

DJ Kflip kuongoza Ma-DJ ujio wa Ne-Yo

MA-DJ kibao wanaotikisa Jembe FM, wakiongozwa na Kevin Michael ‘DJ Kflip’ wanatarajiwa kumsindikiza staa wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’, katika bonge la shoo litakalofanyika Mei 21, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza na Showbiz, mratibu wa shoo hiyo inayotambulika kama Jembeka Festival 2016, Sebastian Ndege alisema kuwa hamu kubwa ya wapenzi wa burudani kwa Kanda ya Ziwa ni ujio wa Ne-Yo hivyo wamejipanga kuweka historia ya aina yake.

“Niseme tu tutakuwa na mastaa kibao Bongo wakiongozwa na Diamond Platnumz. Tutakuwa na Ruby, Maua Sama, Mo Music, Mr Blue, Fid Q, Nature, Stamina, Nay wa Mitego, JJ Band, Skylight Band na wengine kibao,” alisema Sebastian.
Shoo hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom pamoja na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.

Leave a Comment