Oya masela inakuwaje watu wangu wa nguvu? Tudei kama nina kiraruraru hivi maana mizuka ipo juu kinoma. Kitaa hiyo ni mpango? Basi welikamu kwa sana kwenye hizi stori kozi ni tamu kiaje sasa? Kama kawiz niwakumbushe wanakwetu kuwa kitu cha laifu hakitaki mboyoyo mingi arifu.
Kama bado husomeki na kumaindisha mabizinaa yako basi imekula kwako chama langu. Kwenye hili laifu masti mtu unyake unataka nini bati kama umetimba ubaoni kusindikiza wana, mzuka tu kama vepe acha ile kipande yako bati usizingue masela wanaohaso kwa kuwapiga mizinga.
Ebana pipo wana majonzi kinomanoma ya kuondokewa na jembe lao la ukweli kwenye gudi miyuziki ya Bara la Afrika, mtu mzima Papa Wemba. Nasi wana wa hapa jamvini tuseme resti ini pisi kwa mtu mzima Papa Wemba.
Basi bana huku na huku ilikuwa Siku ya Muungano, mtu fedenge nikamingo na bonge moko la sisteri wa kitaa cha bee kutoka waja leo Tanga kunani. Mtoto Cecy pale kati ana msala hatare arifu. Anakuteli kuwa mwanangu huwa chura anamaindisha maji bati siyo maji ya moto!
Ubuyu wenyewe wa kitaa upo hivi; mbebiz mkare aliolewa na mzazi jembe na laifu likawa kwenye levo f’lani za kibabe.
Katika mbishe za laifu selaa wake akawa yupo taiti ileile kwenye kukimbiza ndoto za mafanikio. Kumbe bana huku nyuma kuna kaka mkubwa akawa anamsarendea mai waifu wa jamaa.
Mazee kaka mkubwa akawa anasebenza tu na kujitafunia swala wa jamaa. Si ndo mai waifu wa jamaa akadata? Unaambiwa akaanza kumzingua faza watoto wake hadi akafikia steji ya kumteli kama vepe ammwage tu akafie mbele.
Jamaa naye akaona isiwe kitu, baada ya figisu za deile mtu mzima akaachana na mai waifu wake.
Sasa bana, shori alidhani msela wa mpango wa kando aliyekuwa anampa kichwa atasababisha mambo freshi ya kimaisha.
Ebana kaka mkubwa si ndo akaingia mitini? Shori kumuuliza mtu mzima imekuwaje? Akamteli kuwa alikuwa anamlia mingo kozi alikuwa kwa mume bati kwa sasa hana taimu naye.
Umeona eee…tunapochati hapa jamvini shori yupo njia panda kinoma kozi ameshaharibu kwa faza watoto wake na jamaa aliyekuwa anamsarendea kaingia mitini.
Mmenisoma wana? Samtaimu mtu unapochukua uamuzi f’lani lazima uwe na kitu cha uhakika kozi laifu halikuwa simpo kiivo wanakwetu. Ona sasa shori hana hili wala lile laifu linamshikisha tu adabu!
Kama vepe sii yuu neksti wiki!