Mpendwa msomaji wetu, wiki iliyopita nilianza kuzungumzia mada hii ambayo ni tatizo linalowapata baadhi ya wanawake bila kujijua. Leo tunamalizia kwa kuangalia sehemu ya pili ya tatizo hili ambayo inaitwa Secondary Vaginismus.
Hali hii inatokea wakati mwanamke ndiyo mara ya kwanza anaingiliwa na kitu chochote ukeni na kupata maumivu makali sana. Maumivu haya makali hayatokani na uwepo wa ‘usichana’ bali mwanamke huyu kabla alishawahi kufanyiwa hivyo na hakuwa na maumivu au yalikuwa kidogo lakini sasa anapata maumivu makali yanayompa woga mkubwa.
Maumivu haya ambayo awali hayakuwepo hutokana na maambukizi ukeni hasa fangasi, kuumia baada ya kujifungua mfano kuchanika au kuongezewa njia wakati wa uzazi, lakini wengi hutokana na matatizo ya kisaikolojia au sababu zote kwa pamoja.
Jinsi ya kukabiliana na tatizo hili ni sawasawa tu na lile tatizo la Primary Vaginismus ingawa katika hili itakuwa rahisi kidogo kwa sababu tayari awali hakuwa na tatizo kubwa kama hivi.
Wanawake wanaokaribia ukomo wa hedhi na wale ambao tayari wameshafikia ukomo wa hedhi hupatwa na tatizo hili la kubana misuli ya uke kutokana na umri wao vichocheo vya Estrojeni mwilini kupungua kwa hiyo uke huwa mkavu na kusinyaa na kuwasababishia wawe na uke mkavu hivyo hupata michubuko kirahisi na kuanza kupata maumivu wakati wa kujamiiana na mwisho misuli ya uke inabana.
UCHUNGUZI
Tatizo hili kwa kawaida ni kubwa ingawa kwa kuliongelea huonekana ni dogo au la kawaida. Katika suala la uchunguzi, mwanamke atajijua mwenyewe. Kwanza ni kuguswa au kuingiliwa ukeni kwa hiyo kwa vyovyote vile hayuko tayari.
Inabidi afanyiwe uchunguzi wa kina na awe tayari kukaguliwa ukeni kwa sababu akizidi kuogopa tatizo linaweza kuwa kubwa hivyo kuleta madhara makubwa hasa katika mfumo wa uzazi.
Vipimo vya awali ni daktari kusikiliza historia ya ugonjwa, vipimo vya damu kuangalia homoni hasa Estrojeni endapo italazimu kufanya hivyo na kipimo cha ‘Speculum’ ili kuangalia matatizo ukeni. Maambukizi katika njia ya mkojo na ukeni pia yatachunguzwa.
MATIBABU NA USHAURI
Mgonjwa atatibiwa kufuatana na matokeo ya uchunguzi, matokeo haya ni katika hali ya kisaikolojia, kimwili kwa ujumla Physical hasa kwa wale wanaopata maumivu wakati wa kujamiiana. Katika hali hii mgonjwa atashauriwa afanye mazoezi maalum yaitwayo Kegel au atumie vilainishi vya ukeni kabla ya kuingiliwa viitwavyo K-Y Gel, kujaribu kufanya mazoezi ya kunyoosha misuli ya katikati ya mapaja ili iwe laini upande wa kuelekea ukeni.
Matibabu mengine itategemea jinsi daktari atakavyoona inafaa. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz
