×

Askali Polisi Achomwa Mshale na Mtu Mmoja Aliyegoma Kuhesabiwa Sensa Mkoani Dodoma

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio

ASKARI polisi wa kituo cha Mrijo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma Konstebo William Werema amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa mshale na mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Chioli wilaya ya Chemba mkoani Dodoma aliyegoma kuhesabiwa na makarani wa Sensa.

 

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Nanda Songo mkazi wa kijiji hicho alikuwa anawafukuza makarani wa Sensa waliofika kumuhesabu nyumbani kwake siku ya tarehe 27, Agosti mwaka huu ndipo wakatoa taarifa katika kituo cha polisi Askari walifika na kujaribu kumtibiti lakini aliwashambulia na kumjeruhi Askari huyo tomboni.

 

Akizungumza Askari huyo kutoka katika Hospitali ya Benjamini Mkapa alipolazwa alisema kuwa baada ya kupokea taarifa kwamba mtuhumiwa huyo anahatarisha amani ya kijiji na makarani wa Sensa maaskari akiwemo yeye walijaribu kwenda kumkamata.

Konstebo William Werema amelazwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Doddoma

“Ilikuwa Agosti 28, tulipata taarifa kwa wananchi kuwa kijijini kwao kuna mtu anatishia  watu kwa kwa mishale, sisi kama jeshi la polisi tuliokabidhiwa jukumu la kulinda wananchi tulifika na kuwasaidia”

 

Aliongezea kwa kusema kuwa walipofika nyumbani kwake kumkamata hawakumkuta ghafla alitokea kichakani na kuanza kurusha mishale ovyo ambapo mmoja ulimpata  maeneo ya tumboni.

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji cha Manyata kijijini hapo, huku akisema kuwa Askari huyo alichomwa kwa mshale unaodhaniwa kuwa na sumu na Nanda Songo (45) ambaye alifariki dunia kwa kupigwa risasi maeneo ya kifuani na mguu wa kulia wakati akiwashambulia Askari kwa sababu aligoma kujisalimisha.

 

Pia alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na mishale 23, pinde mbili, visu viwili, Ala ya kuwekea mishale, dawa mbalimbali za kienyeji na hati ya kumaliza kifungo katika gereza la King’ang’a wilayani Kondoa, alikuwa mfungwa namba 46/2022 kuanzia Agosti 23, 2021 hadi February 11, Mwaka huu.

 

Imeandikwa na Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment