
Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA| MAKALA
KWA mara ya kwanza tangu aanze muziki, staa wa Bongo Fleva, Elly Michael ‘Y Tony’ ameweza kushaini katika TV kubwa ya Ufaransa, Trace Urban baada ya video ya wimbo wake wa Wivu kuanza kuchezwa.
Akichonga na E’bana Dah, Y Tony aliyewahi kubamba na Wimbo wa Masebene alisema kuwa, Bongo kuna wasanii wengi lakini ni wachache sana wanaopata bahati ya nyimbo zao kuchezwa kwenye TV hiyo kubwa nchini Ufaransa.

“Nimefarijika sana, nimezoea kuona wakali wa Sauz na Nigeria kama Cassper Nyovest, AKA, P Square, Wizkid wakichezwa kwenye TV hiyo lakini sasa muziki wetu umesogea na nashukuru nimekuwa miongoni mwa wakali wanaochezwa huko,” alisema Y Tony.
Wakali wengine ambao nyimbo zao zilishawahi kuchezwa katika TV hiyo ni Darassa, Diamond, Belle9 na Joh Makini.