Msomaji wa Gazeti la Amani, Juma Seif (kushoto) akijaza kuponi ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Shabani Ramadhan (kushoto) naye akijaza kuponi yake ili kushiriki bahati nasibu hiyo.

Msomaji wa Amani (katikati), Haji Maulid akielekezwa na Ofisa Masoko, Yohana Mkanda namna ya kukata na kujaza kuponi yake.

Mdau wa Gazeti la Amani, Katanga Mgalule (kushoto) naye akijaza kuponi yake.

Ally Kassim akijaza kuponi yake katika Gazeti la Amani ili kushiriki droo ndogo ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda akimshuhudia msomaji wa Gazeti la Amani, Ramadhan Ally akijaza kuponi yake.

Ramadhani Kijao (kushoto) akikata kuponi yake baada ya kujaza ili kushiriki droo hiyo.
Msomaji wa Amani akielekezwa na Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub (katikati) namna ya kujaza kuponi.
ZIKIWA zimebaki siku 28 mshindi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kuimiliki nyumba hiyo, wasomaji wa Gazeti la Amani katika maeneo ya Kisarawe, Pwani na maeneo mengine leo wameonekana kuvutiwa nayo baada ya kujaza kuponi nyingi ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda.
Bahati Nasibu hiyo inayoendelea kutisha hapa nchini, inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kupitia Magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Gazeti pendwa la Michezo la Championi.
Afisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda alisema: “Siku zinazidi kuyoyoma na mshindi wa nyumba hiyo anaweza kuwa wewe, hivyo nunua magazeti ya Global mengi na kujaza kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda.”
Na Denis Mtima/GPL

