×

Dk. Cheni alia na serikali

DKCHENI51.jpgBoniphace Ngumije,

Risasi Jumamosi

MUIGIZAJI nguli Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ametoa ya moyoni kwamba serikali haisimamii vizuri kazi zao kwani zimekuwa zikiendelea kuoneshwa kiholela pasipo wasanii kuingiza kipato.

Akichonga na gazeti hili, Dk. Cheni alisema tatizo hilo ndilo lililosababisha asuesue kwenye kazi yake hiyo kwani licha ya kuahidi kupambana na maharamia, uoneshwaji hovyo wa kazi zao, bado ni tatizo linalozidi kushika kasi.

“Mianya bado ni mingi. Maharamia wanaendelea kudurufu filamu. Bado zinaoneshwa kiholela kwenye vibanda umiza. Serikali inatakiwa kudhibiti mianya yote ya watu wanaotumia kazi zetu kwa manufaa yao binafsi ili wasanii tuondokane na umaskini,” alisema Dk. Cheni.

Leave a Comment