×

Meninah Apigwa ndoa ya pili!

Menina ndoa

Menina ndoa ya pili.

ANDREW CARLOS

BAADA ya kuachana na mumewe wa kwanza aliyejulikana kwa jina la Abdulkharim Haule, ishu nyingine imeibuka kuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Meninah Abdulkareem ‘Meninah’ amepigwa ndoa ya pili.

Menina-ndoaMenina ndoa ya kwanza.

Akizungumza na Over Ze Weekend, meneja wa Meninah ambaye pia ni kaka yake, Atik alithibitisha kufungwa kwa ndoa hiyo wikiendi iliyopita na kuwa imekuwa ni jambo jema kwao.

“Hatupendi mambo yaende kiuwazi sana, ndoa ya kwanza ya Meninah ilifungwa kimyakimya na hii tumefanya hivyo. Ndoa imefungiwa nyumbani (Kigamboni, Dar) na aliyemuoa wala siyo mtu maarufu ni mtu wa kawaida tu,” alisema Atik.

Agosti mwaka jana, Meninah alifunga ndoa ya kimyakimya na Haule ambayo haikudumu kwani ilivunjika miezi michache baadaye.

Leave a Comment