×

Ramadhani Tukufu Iwe ya Huruma kwa Watanzania

Kiongozi wa Chuo cha Kiislamu cha Hawaza Imam Swadiq ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Waislamu wa Shia Ithna Asherri Tanzania, Sheikh Hemed Jalala (2)

Kiongozi wa Chuo cha Kiislamu cha Hawaza Imam Swadiq ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Waislamu wa Shia Ithna Asherri Tanzania, Sheikh Hemed Jalala.

Viongozi wa Dhehebu la Shia wakiwa kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani)

Viongozi wa Dhehebu la Shia wakiwa kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani) wanahabri wakiwa kaziniKiongozi wa Wanahabri wakiwa kazini

Chuo cha Kiislamu cha Hawaza Imam Swadiq ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Waislamu wa Shia Ithna Asherri Tanzania, Sheikh Hemed Jalala leo amewatakia mfungo mwema Waislamu na wasio Waislamu pamoja na kusisitiza kudumisha amani katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Kigogo Post jijini Dar, amewataka Waislamu na wasio Waislamu kuutumia mfungo wa Mwezi wa Ramadhani kuwa ni wa matendo ya huruma kwa yatima, wajane, wagonjwa, wasiojiweza na kukemea matukio ya kinyama ambayo yametokea sehemu mbalimbali za nchi ikiwemo mauaji ya watu saba waliochinjwa mkoani Mwanza, katika msikiti wa Buhongwa, Tanga na kwingineko.

“Ndugu zangu Waislamu na Wakristo wote tuutumie mwezi huu huu katika kufanya matendo ya kumpendeza Mwenyezi Mungu, matendo ya huruma kwa wajane, yatima, wasiojiweza, wagonjwa na tukemee vikali mauaji ya kinyama yanayoendele nchini,’’alisema Jalala.

Na Gabriel Ng’osha/GPL

Leave a Comment