Wachezaji wa Yanga wakipambana na wachezaji wa TP Mazembe jana.
KATIKA kuonyesha kuwa wamejipanga vyema na michuano ya kimataifa uongozi wa klabu ya Yanga imetumia zaidi ya shilingi milioni 260, katika kambi yake ya Uturuki ikiwa ni maandalizi ya michezo miwili ya Mo Bajaia na TP Mazembe.
Yanga ambayo imefuzu kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano hiyo baada
ya kuwaondoa Sagrada Esparanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1, jana Jumanne ilicheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mo Bajaia ya Algeria kwa kufungwa bao 1-0.
Kabla ya kuanza hatua hiyo ya makundi uongozi wa timu hiyo uliamua kuipeleka timu nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi yake ambapo uchunguzi uliofanywa
na gazeti hili umebaini kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika maandalizi yao ambayo wamekaa nchini humo kwa zaidi ya siku kumi.
“Gharama ni kubwa ila uongozi ulipanga timu ikafanye maandalizi katika mazingira bora hilo halikuwa tatizo kwa sababu usafi ri wa ndege kwenda na kurudi peke yake zimetumika dola elfu 60, ambayo sawa na milioni 127 yaani hapo ile safari ya kwenda Algeria kucheza na Mo Bejaia haipo
gharama zake.
“Unajua hata kule timu ilikuwa inakaa katika hoteli ya kisasa ambayo uongozi umetumia kulipa kiasi cha euro elfu 58 ambazo ni sawa na milioni 137, kwa wakati wote timu ilivyokuwa huko, nadhani jumla yake inafi ka kama milioni 260,” kilisema chanzo hicho. Katika mchezo wa kwanza Yanga ilikutana na Mo Bejaia ya Algeria huku ikiwa imetokea Uturuki ilipokuwa imeweka kambi ambapo ilipoteza mchezo huo kwa bao 1-0.
