Harakati za hapa na pale zikiendelea katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo jijini Dar.
Wananchi wakifanya maandalizi kuelekea sikukuu ya Eid El Fitr.
Harakati za hapa na pale ndani ya mitaa hiyo zikiendelea.
Taswira ya moja ya mtaa uliokutwa una watu wengi wakiwa ‘bize’.
Kamera yetu leo imeshuhudia mamia ya watu wakiwa wamefurika kwenye mitaa ya Kariakoo, hususan Mtaa wa Congo, wengi wakifanya manunuzi ya nguo na mahitai mengine, ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya Eid el Fitr inayotarajiwa kusherehekewa kesho (Jumatano) au keshokutwa (Alhamis).
Tofauti na siku nyingine zote,, idadi ya watu ilionekana kuongezeka zaidi katika siku hizi za kuelekea Sikukuu, jambo lililowalazimu Jeshi la Polisi kuongeza ulinzi kwenye mitaa hiyo, ikiwa ni sambamba na zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo ‘wamachinga’.
Pichani ni mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kama walivyokutwa Mtaa wa Congo, Kariakoo leo.
DENIS MTIMA NA HASHIM AZIZ/GPL













