×

Rayuu akacha shisha

RAYUUMAYASA MARIWATA

MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ aliyewahi kuripotiwa kuwa mtumiaji mzuri wa kilevi cha shisha, amesema kuwa, kwa sasa hatumii kilevi hicho na isitoshe kitendo cha kupigwa marufuku na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kimemkosha mno.

Akipiga stori na Amani, Rayuu alisema watu wengi wanafikiri kuwa yeye ni mwanachama wa kilevi hicho kumbe ameshaacha siku nyingi na isitoshe alikuwa akionja tu mara mojamoja na ndiyo maana kaweza kuacha kirahisi.

“Nilikuwa nikionja tu wala sina uzoefu nacho, nimefurahi sana ilivyopigwa marufuku maana kuna mtu wangu wa karibu anakipenda sana hadi ananiboa, wanaotumia bora waache kwani kina madhara,” alisema Rayuu.

Leave a Comment