×

Dkt. Abbasi: Rais Samia Ameanza Kuipa Thamani Sekta ya Ufugaji Nyuki

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeanza kuchukua hatua madhubuti kuipa thamani Sekta Ndogo ya Ufugaji Nyuki nchini.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Novemba 8, 2024, alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafali ya 28 ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI) kilichopo Tabora Mjini.

Akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Rais Samia kuwa ni pamoja na kuiingiza Sekta ya Ufugaji Nyuki kwenye Mpango Kabambe wa BBT ambapo sekta hiyo itapata msukumo zaidi wa raslimali fedha, watu na kutengeneza kipato kwa wananchi.

“Jambo kubwa la pili, kutokana na hilo la kwanza, Wizara nayo imekamilisha Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Ufugaji Nyuki utakaoitwa ‘Achia Shoka, Kamata Mzinga’,” alisema Dkt. Abbasi akisisitiza mipango hiyo itatoa ajira zaidi na kipato kwa wananchi na kuongeza mchango wa sekta ya misitu na nyuki kutoka asilimia 4.3 ya sasa katika Pato la Taifa.

Jumla ya wanafunzi 210 wamehitimu chuoni hapo leo na kuongeza wataalam wa sekta hiyo nchini ambapo kati yao 110 wamemaliza ngazi ya Cheti na 100 Diploma katika taaluma za ufugaji nyuki.

KUFUNGWA kwa YANGA HAMISA MOBETTO ATAJWA-PATRICK KANUMBA KUTOKA KIMAPENZI na NANA AFUNGUKA

Leave a Comment