BAADHI ya wasomaji magazeti wamelichangamkia gazeti bora la Ijumaa ambalo linaongoza kwa kuandika habari za mastaa wa Kibongo na Mamtoni katika maeneo ya Makongo Juu na Goba, Dar.
Katika promosheni ya mauzo iliyofanyika kwenye maeneo hayo ikiongzwa na Afisa wa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda ambao ndiyo wachapishaji wa gazeti hilo
Adelina Felix akisoma gazeti la IJumaa ambalo lipo katika muonekano mpya kwenye eneo la Makongo Juu.
Wasomaji hao ambao walikuwa wakinunua gazeti hilo ambalo walionekana kuvutia nalo kutokana na kuwa katika muonekano bora na wa kisasa huku likiwa limesheheni habari kibao za mastaa mbalimbali.
Msomaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Kisauti akilisoma gazeti la Ijumaa kwa umakini katika eneo la Goba.
Msomaji Hawa Saidi akisoma gazeti la Ijumaa akiwa ndani ya duka lake katika eneo la Makongo Juu.
Zebedayo Tito akiwa anasoma gazeti la Ijumaa katika eneo la Goba.
Msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Maria Tuluka akipewa maelekezo wakati anasoma gazeti la Ijumaa na Afisa Masoko wa Global Publisher, Yohana Mkanda katika eneo la Makongo Juu.
NA JIMMY HAROUB/GPL
