×

Mwingereza Afungwa Miezi 12 Kwa Kutaka Kumuua Trump

mwingereza-afungwa-miezi-12-kwa-kutaka-kumuua-trumpRAIA mmoja wa Uingereza amefungwa miezi 12 na siku moja gerezani katika jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Republican,  Donald Trump ambaye kwa sasa ni Rais Mteule wa Marekani.

Michael Sandford, mwenye umri wa miaka 20, alikiri kosa hilo mnamo Septemba akiwa kwanza anaishi kiharamu nchini humo na kwa kutaka kuvuruga hafla ya kiserikali.  Mtu huyo alishitakiwa kwa kumpora polisi bunduki kwenye mkutano huko Las Vega ili amuue Trump.

Sandford, anayeishi Dorking, Surrey, alikuwa anakabiliwa na kifungo cha kufikia miaka 10 gerezani kwa njama hizo.

Hata hivyo, mahakama ilisema anaweza kuachiliwa baada ya miezi minne na atarudishwa Uingereza ambapo upande wa utetezi ulisema pia kwamba mtu huyo ana matatizo ya akili.

Darassa Afunguka Tuhuma za Kuiba Beat ya Saida Karoli Kwenye Wimbo Wake wa Muziki