Na Musa Mateja | Global Publishers
Taarifa zilizotufikia zimeeleza kuwa, msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu hajafikishwa mahakamani Kisutu leo Leo February 8, 2017 kwa madai kuwa amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali leo kwa ajili ya kupimwa na kuthibitisha iwapo anatumia madawa ya kulevya au la!
Imedaiwa kuwa, Polisi Dar, wamefikia hatua hiyo baada Wema kukana kutumia madawa wakati alipokuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi.
Taarifa zimedai kuwa mastaa wenzake kama TID na wengine walikiri kutumia madawa na kupewa onyo kali huku mahakama ikiwapa masharti matatu likiwemo la kuripoti polisi mara mbili kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja na kuwa chini ya uangalizi wa mahakama, kisha kujidhamini kwa bondi ya shilingi milioni moja na kurudi uraiani wakati Wema akikana kutumia madawa.
Taarifa zaidi zimedai kuwa, polisi wanaendelea kumshikilia Wema huku wakisubiri ripoti ya mkemia mkuu ili waweze kukamilisha upelezi na kumchukulia hatua zinazostahili.
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa jeshi lake bado linamshikilia Wema na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo na kuwa jalada lao limepelekwa kwa wakili wa selikali alipitie ili aone ushahidi uliopo pamoja na kupata majibu kutoka kwa mkemia mkuu wa selikali kubaini kama kweli ni mtuamiji wa madawa ya kulevya.