Dalili Hatari kwa Wajawazito
Imewekwa na on February 11th, 2017 , 06:05:30am

Dalili Hatari kwa Wajawazito

Na DOKTA WA RISASI| MTANDAO|RISASI JUMAMOSI| MAKALA

na Mitandao WAJAWAZITO wengi huugua wakati wakiwa na ujauzito. Zipo sababu zinazofanya kutokea kwa maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba. 

Kuna matatizo mengi  yanayohusiana tu na mimba, hata hivyo ni muhimu kukumbuka kwamba hali yoyote ambayo husababisha maumivu kwa mgonjwa asiyekuwa na ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito. Tofauti kati ya watu hao wawili hupatikana baada ya uchunguzi.  Maumivu ya tumbo kwa mjamzito  ni changamoto

kwa sababu wengi hupatwa na  kichefuchefu, kutapika, na maumivu ya tumbo hujitokeza mara nyingi. Mfuko wa uzazi unapotanuka unaweza kusukuma  viungo vingine kando ndani ya tumbo, upungufu wa damu na leukocytosis ni kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa vya upungufu wa  damu au maradhi.   

Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi, kinaweza kusababisha maumivu ya tumbo ambayo huchukua muda wa siku mbili au tatu na kiasi kidogo cha damu  ukeni hutoka. Mara nyingi kiasi hiki cha damu huwa ni kidogo na

hutokea kati ya siku saba au 12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa, mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa anatarajiwa kuingia hedhi. Hivyo, wagonjwa  mara  nyingi hufanya makosa kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida.

Mimba iliyotunga nje ya mfuko: Tatizo hili husababisha maumivu kwa akina mama wengi walio na mimba nje ya mfuko wa mimba. Tatizo hili linaweza kubainika kwa kutumia Ultrasound na kipimo cha homoni HCG. Uzuri ni kwamba tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji.

KUTOKA KWA MIMBA

Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo vya akina mama katika nchi zinazoendelea.

Uvimbe kwenye mirija ya mayai (Ovarian cyst): Wakati mwingine uvimbe huu hupasuka au kujizungusha. Hata hivyo, unaweza kupungua na usipopungua unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa ujauzito. Sababu nyingine ni kujizungusha kwa mirija ya mayai (Ovarian torsion). Hii hujitokeza mara chache. Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa mkubwa.

Itaendelea wiki ijayo

Save

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma