
Na SOPHIA MA`MDOGO| GAZETI LA UWAZI| LOVE & LIFE
HAYA tena shoga yangu leo ndiyo kumekucha peupeeee! Ni Jumanne nyingine tena tumekutana katika kona yetu hii ya mashamsham, kona pendwa kati ya magazeti yote yanayoandika mahabati. Kwanza shoga u mzima maana siyo umekodoa mijicho kunisoma bila kujuliana hali?
Mwenzako mimi nimejaa tele kama treni ya abiria ila kama ni mgonjwa siku zote huwa nawaombea jamani uongo? Basi ugua pole najua Mwenyezi Mungu atatia wepesi na utakuwa mzima! Baada ya kusema hayo kwanza nikupongeze wewe shoga yangu uliyesherehekea Sikukuu ya Wapendanao ukiwa na mpenzi wako. Najua umezingatia yale niliyokuwa nimeandika wiki iliyopita.
Kwa wale mlioumizwa na mapenzi na wengine kusalitiwa niwape pole kwani mapenzi ndivyo yalivyo jamani, wanaume wa siku hizi wamebadilika, wengine wanasingizia hawana pesa kumbe wana lao jambo, looh! Haya nisijeonekana muongeaji sana wakati najua kabisa hamu yako ni kujua hizo sehemu tano za kumpagawisha mwanaume wako ni zipi.

Shoga mwenzako nimekuwa nikipokea meseji nyingi, mara ohh; Anti naomba unifunze! Anti naomba njia za kumpagawisha mume wangu, jamani mambo mengine ni utundu siyo lazima kufundishwa, upo? Ngoja nianze kwa kukung’ata sikio kwanza kidogo! Shoga wanaume nao huwa wana maeneo ya kuwasisimua na kuwapeleka katika dunia nyingine, nadhani nikisema dunia nyingine umenipata, upo? Leo nitayataja maeneo ambayo mzee kabla hajala chakula cha usiku akiguswa kama siyo kupetiwapetiwa lazima yamsisimue sana na kumfanya ahisi dunia yote yake ati!
MASIKIO
Shoga kama ulikuwa hujui na hili basi chukua jembe na mbegu ukalime ukirudi upike na ulale maana loo si kwa ushamba kama huu! Mzee anapenda mwanamke mtundu, anayejua kupatiwa hisia sehemu za mwili wake ati, siyo umekaa kaa kama kinyago cha mpapure, upo somo?
Ukifika muda wa chakula cha usiku, shoga mara kwa mara hebu uwe unafanya kama kumnong’oneza kama siyo kumuhemea masikioni kwake uone! Tena shoga usisahau kutumia ulimi au pindo la kanga lenye umatemate, umenipata?
SHINGONI
Hivi shoga unajua kwamba mishipa mingi ya fahamu kwa binadamu hukutania shingoni? Sasa hapo shoga ndiyo pakuchezea ili mishipa hiyo iende sehemu yake, upo somo?
Ila nawapa somo kwa wale wazee ambao wao hupenda kula chakula cha usiku wakiwa hawajakoga, mijasho ya siku nzima looh! Shoga raha ya shingoni uwe msafi, shingo imekatika kama siyo kuteleza, umenipata? Tena kuna kale kamchezo kakung’atana Wazungu wanaita love bite, usipitwe shoga maana kama nakuona unavyosoma kwa makini, hujui love bite wewe?
Wapo wanaopenda kuwekewa lakini wengi hawapendi shoga maana unaweza kumsababishia matatizo ofisini au sehemu za kuheshimika upo? NGOZI Shoga hapa ujue kucheza na ngozi, vinyweleo vyako na vyake.
Sasa kama wewe mwenzangu na mimi mkono wako mgumu kama kokoto za mabondeni basi jifunze kupaka hata losheni kukwepa aibu, umenipata shoga? Asikwambie mtu shoga, hamuwezi kula chakula cha usiku bila kuserereka na mikono, kupitisha huku na kule, hee heee heiyaa! Shoga kushikana huku humfanya mzee mzunguko wake wa damu kuongezeka na kuwa wenye kasi na kumsaidia baadhi ya maeneo kuchachamaa na kufanya kazi vizuri.
Siri ya ngozi shoga ni kuhifadhi pumzi, wengi wamekuwa wakitumia njia hii ya kupapasa kama siyo kushika ili wazee wao wasichoke kula chakula cha usiku.
MABUSU
Utakuwa unajiuliza shoga hayo mabusu vepeee? Shoga siyo mabusu ya kumpiga mtoto ati! Hapa namaanisha mabusu ya kiutuuzima upo? Mzee anatakiwa kupigwa mabusu mazito, mabusu ya kuanzia nusu lita hadi lita moja, upo? Unaweza kumpa mabusu sehemu nyingi kadiri uwezavyo na ukiona amezubaa basi ndipo anapopendelea mzee, umenipata shoga yangu ehhh?
KUCHA
Hili nalo neno shoga? Wazee wa siku hizi siyo wa zamani, hawa wanawaita wa dijitali, wa kisasa kama siyo waulayaulaya, umenipata? Shoga chakula cha usiku kinacholiwa bila kucha kufanya kazi yake hicho kinaweza kuwa kama siyo kimechacha basi hakijaiva vizuri.
Shoga usishangae wengine wanafuga kucha ukajua urembo, kucha zina siri yake babu weee kama ulikuwa hujui jua sasa! Mwanamke sharti ujue kutumia kucha kuanzia shingoni, mgongoni hadi kwenye nyayo upo? Kwa leo niishie hapa wangu, kwa ushauri na kujifunza zaidi nicheki kwenye namba yangu hapo juu, usibipu babu weee, tuma meseji nitajibu!