×

Chirwa Anyoa Upara Awafunge Azam FC

Wilbert Molandi |CHAMPIONI IJUMAA| Dar es Salaam

STRAIKA wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa, amebadili mwonekano mpya kichwani kwake baada ya kunyoa nywele zote huku ikielezwa ni kutoa mikosi ili awafunge wapinzani wao Azam FC.

Yanga na Azam zinatarajiwa kukutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Mzambia huyo amekuja na staili hiyo huku akiachia ndevu, muonekano ambao ameanza kuonekana nao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Rafiki wa Chirwa ameliambia gazeti hili kuwa Chirwa ameipania mechi dhidi ya Azam, hivyo amepanga kufanya kila jitihada kuhakikisha anawafunga kisha bao atakalofunga liwe zawadi kwa mtoto wake aliyezaliwa wiki iliyopita.

Alipotafutwa Chirwa kuzungumzia hilo alisema:  “Sitaweza kuongea hadi nikapopata ruhusa kutoka kwa kocha.”

Lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram alitupia picha yake akiwa mazoezini akiwa na upara na kuandika ‘new look’.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.