×

AMANDA: Tatuu ni Kama Teja wa Unga

Amanda Poshi.

Na MWANDISHI WETU| RISASI MCHANGANYIKO| RISASI VIBES

MWANADADA kutoka Bongo Muvi, Amanda Poshi ameibuka na kusema kuwa kuchora michoro mwilini ‘tatuu’ ni kama teja wa madawa ya kulevya ‘unga’ kwani ukijaribu moja, unatamani ujaze mwili mzima.

Akizungumza na Risasi Vibes, Amanda alisema wakati anachora tatuu ya kwanza mwilini mwake, alisema atakuwa nayo hiyo tu, lakini siku zilivyozidi kwenda akajikuta akiongeza mpaka sasa zimefika tano na bado anatamani kuongeza nyingine hivyo anawasihi watu ambao hawajajichora, wasijaribu kuanza.

“Nawasihi wale ambao hawajawahi kuchora wasijaribu kwani hii ni kama teja wa unga, maana ukishachora moja utatamani uongeze na nyingine, kuhusu kwamba namkosea Mungu, mimi naona dhambi zote ni sawa tu maana hata wanaofanya ukahaba hata kwenye maandiko imekatazwa lakini wanafanya hivyo,”

Leave a Comment