×

Presha Yataka Kutoa Uhai wa Lungi

Na Hamida Hassan | IJUMAA | STAR MIX

STAA wa fi lamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga ameibuka na kusema kuwa presha ilitaka kuondoa uhai wake kwani alijikuta akiamka asubuhi akiwa amevimba mwili mzima na nguvu hana.

Akizungumza na Ijumaa, Lungi alisema kuwa, hali hiyo ilimjia juzi ambapo ilibidi akimbizwe Hospitali ya Mico iliyopo Kinondoni jijini Dar alikolazwa kwa ajili ya matibabu.

“Ama kweli tunatembea na kifo, presha ya kushuka inanisumbua sana na cha ajabu nilipoamka niliona mwili umevimba, namshukuru Mungu sasa naendelea vizuri,” alisema Lungi.

Leave a Comment