×

Pam D, Gigy Money Kukalishana Dar Live

 

Gift Stanford ‘Gigy Money’.

GAZETI LA AMANI | SHOWBIZ EXTRA | DAR LIVE

WAKATI ikiwa imesalia siku moja kufikia Mei 6, King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuwa refa katika mpambano wa kukalishana kwa kuimba kati ya Pamela Daffa ‘Pam D’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, shoo nzima inatarajiwa kuanza saa mbili za usiku ambapo Bella pamoja na bendi yake ya Malaika wataanza kwa kutoa burudani ya nguvu kwa kupiga nyimbo zao zote kali.

Msanii wa Bongo Fleva, Pamela Daffa.

“Mashabiki wajipange na wajiandae kwa shoo ambayo tangu mwaka uanze Bella hajawahi kufanya. Hiyo ni fursa kubwa mashabiki wote wanaoizunguka Dar Live na Dar es Salaam kwa ujumla. “Usiku huo zitapigwa nyimbo zote kuanzia Yako Wapi Mapenzi, Nashindwa, Nani Kama Mama, Msaliti, Nishike na nyingine kibao,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa Sh.7,000 tu.

King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’

Naye Bella alitia neno kuwa kwa mara ya kwanza tangu aanze muziki atakuwa refa katika mpambano wa Gigy Money na Pam D ambapo bingwa atapata tiketi moja kwa moja ya kutengeneza naye kolabo na video.

“Wote wanaju-likana  kama ni wasanii ambao ni wazuri. Kila mmoja ana jina hivyo ni wakati wa wewe shabiki kuamua nani unaona anafaa nifanye naye kolabo. Usiku huo mshindi nitamvalisha ‘crown’ maalum,” alimaliza.

Leave a Comment