
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameikabidhi bendera timu ya Azania Company ambao mabingwa wa Kanda wa Bank ya Standard Chartered Afrika Mashariki na Kati.
Waziri huyo alikabidhi bendera katika hafla fupi ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika leo kwenye Hotel ya Southern Sun, Posta jijini Dar es Salaam.

Azania wanatarajiwa kuelekea nchini Uingereza Mei 15, mwaka huu kwa ajili ya kwenda kupambana na kanda za nchi za Africa Magharibi na mataifa mengine ulimwenguni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwakyembe alisema anawatakia kila la kheri Azania katika mashindano hayo na kikubwa amewataka wachezaji hao kupambana na kuchukua ubingwa huo.

“Kwanza nianze kwa kuwapongeza waandaaji Standard Chartered Banki kwa kuandaa mashindano hayo makubwa yatakayofanyika Anfield, Uingereza na Tanzania kutoa mwakilishi Kanda ya Afrika Magharibi.
“Kikubwa vijana wetu ambao ndiyo wawakikirishi wetu Tanzania muhende kuiwakilisha vema nchi kwa kurudi na ubingwa.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Fedha Kigeni wa Standard chartered, Abdulrahman Said alisema mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Mei 21 mwaka huu na Azania wenyewe watakuwa kundi moja na timu ya Botswana, Nigeria, Korea, Hong Kong, Singapore na Uingereza.
Said alisema, timu hiyo baada ya mashindano watatembelea Uwanja wa Anfield unaotumiwa na Liverpool.