×

Hawa Jamaa Wamevurugwa Hatari

Daniel Ndambuki

 

UZALENDO ni kukubali kilicho chako hata kama kibaya. Lakini si dhambi kusifia cha mwenzio kizuri. Nasema hivyo kwa sababu katika tasnia ya burudani Afrika Mashariki, upande wa vichekesho Kenya na Uganda zinatuchapa fimbo na hatuna budi kuzisifia.

 

Zinatuchapa kwa sababu tayari zinamazao ya vijana waliofanikiwa zaidi kwenye tasnia hiyo na kujitengenezea ‘fun base’ kubwa kiasi kwamba huwezi kutaja wachekeshaji bora wa komedi Afrika Mashariki na usiwataje Daniel Ndambuki ‘Churchill’, Eric Omondi, Professor Hamo, MC Jessy, MCA Trick, Anne Kansiime, Salvador, Teacher Mpamire na wengine kutoka nchi hizo.

 

MC Jessy

 

Hawa jamaa wamevurugwa kwelikweli. Wakishika maiki ni lazima watakuacha unashika mbavu zako kutokana na ubunifu wa kile watakachokifanya jukwaani.

 

Hata hivyo, ingawa wachekeshaji hawa wa vichekesho vya majukwaani ‘stand-up comedy’ wanabeba sifa siyo kwamba kwetu Bongo hawapo.

Wapo wengi tu ambao ni akina Evance Bukubuku, MC Pilipili, Idris, Mpoki, Katarina, Mkaliwenu na wengineo lakini bado wanaonekana kuwa nyuma kwenye tasnia hiyo.

 

 

Eric Omondi

 

Huwezi kuwalinganisha wasanii hawa na Eric Omondi pekee ambaye amewahi kualikwa kwenye shoo kubwa ya komedi duniani iitwayo The Tonight Show ya muigizaji maarufu Marekani, Jimmy Fallon.

 

Eric na wenzake niliowataja hapo wapo mbele na kuna haja ya wasanii wetu wa Kibongo wa vichekesho kujifunza baadhi ya vitu kutoka kwao ili waweze kufanikiwa kuitoa komedi kwenye maharusi na kuifanya iwe shoo rasmi ya kukusanya watu ambao wanakuwa tayari kuchangia pesa kutokana na burudani wanayoipata.

 

Anne Kansiime

 

 

Mambo ya kujifunza

Miongoni mwa vitu ambavyo wasanii wa Bongo wanatakiwa kujifunza kwanza ni juu ya ubunifu wa vichekesho vyao. Ubunifu utawasaidia kina Pilipili kuepukana na lawama kuwa wanatafsiri vichekesho vya akina Basket Mouth ambavyo watu wamevisikia tangu mwaka 2008. Hapa nyumbani kuna vitu vingi mno pamoja na matukio ya kuelezea na yakachekesha watu kama anavyofanya MCA Tricky anapokuwa anachambua mambo yanayotokea nchini kwake Kenya kwenye vichekesho vyake.

 

 

MC Pilipili

 

 

Menejimenti

Hili nalo ni muhimu zaidi. Eric Omondi hadi amefika hapo amekuwa na back-up kubwa ya Daniel Churchill na menejimenti yake kabla hajajiengua.

 

Menejimenti itawasaidia katika kubuni vichekesho vinavyoendana na wakati na kuwa na mikakati thabiti ya kuhakikisha kile msanii anachokifanya kinawafikia walaji.

 

Idris

 

Nakumbuka Kibongobongo, Evance Bukubuku ni miongoni mwa wachekeshaji waliojaribu kufanya hiki ninachokielezea hapa. Aliwahi kuwa na kundi la komedi liitwalo Vuvuzela na alikuwa na menejimenti nzuri tu ambayo ilimsaidia kuandaa vipindi na matamasha ya komedi kabla ya kundi hilo kuvunjika na wasanii wake kina Dogo Pepe, Maganiko kusambaratika.

 

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo wasanii wetu wanatakiwa kujifunza na wakiyafanyia kazi na kuwa na bidii watafika mbali na kututoa kimasomaso.

 

Makala: Boniphace Ngumije | UWAZI

 

Prof. Jay na Mkewe Walivyoanza Kuonja Utamu wa Keki kwa Staili Hii

Leave a Comment