
KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) imeiweka hadharani mikanda itakayogombaniwa katika mapambano ya Tubing wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika Julai 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar.
Katika mapambano hayo ya kimataifa yatakayorushwa mubashara na Kituo cha Global TV Online kupitia webiste yake ya www.globaltvtz. com, Bondia wa Tanzania, Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ atapambana na Israel Kamwamba wa Malawi.
Pambano lingine litakuwa ni kati ya Idd Pialali dhidi ya Regin Champion raia wa DR Congo, wakati Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ atacheza na Tinashe Mwadziwana kutoka Zimbabwe. Mapambano hayo yote ni ya raundi kumi.
Rais wa TPBO, Yassin Abdallah ‘Ustaadh’, ameitambulisha mikanda itakayogombaniwa katika mapambano hayo huku akithibitisha uwepo wa Balozi wa Malawi wa hapa nchini, Hawa Ndilowe kwenye pambano hilo.
“Maandalizi ya mapambano ya kimataifa, kati ya mabondia wa kutoka DR Congo, Malawi na Zimbabwe ambao watapigana na mabondia wetu hapa, yamekamilika. Kila kitu kimeshakuwa sawa na wameshapata barua maalum kutoka katika mashirikisho ya nchi zao.
“Huo ndiyo mfumo wa ngumi za kulipwa unavyokuwa, bondia anatakiwa apate ridhaa na kibali cha kwenda kupigana nje ya nchi kutoka kwa kamisheni, chama au shirikisho la ngumi za kulipwa ndani ya nchi yake.

“Lakini jambo lingine la heshima ni kuwa nimepata uthibitisho kutoka kwa ndugu zetu wa Malawi kuwa balozi wao, Hawa Ndi l owe ambaye y u p o h a p a n c h i n i atakuwepo kushu h u d i a n d o n g a hizo.
“ L a b d a niwaambie ma b o n d i a wa Tanzania ambao w a t a c h e z a katika mapambano hayo ya ubingwa na mabondia kutoka nje, najua wanajiandaa vizuri lakini natoa onyo kwao kwamba hawa mabondia wanaokuja siyo legelege hata kidogo.
“Tumeleta mabondia wa ukweli kwa sababu hili pambano litaonyeshwa live kupitia Global TV Online maana Watanzania siku zote wanapenda vitu vizuri, vya ukweli na hawapendi kuona vitu feki.
“Licha ya hivyo sisi kama viongozi tupo katika mipango ya kuujenga mchezo wa ngumi za kulipwa kwa Watanzania ili tujenge uaminifu zaidi kwa wadau wa mchezo huu hapa nchini, ieleweke kuwa mchezo huu ni wa pili kwa ukubwa hapa kwetu.

“Mashabiki wote ndani na nje ya nchi wajue kuwa pambano hili halitakuwa kama ilivyozoeleka katika mapambano mengine.
“Kiukweli hatutahitaji watu wengi ndani ya ukumbi kwa sababu wale ambao watapata fursa ya kuja ndani ya ukumbi pale Dar Live watakuwa wana kadi maalum za mialiko na wengine ambao hawataweza kupata kadi hizo wataangalia kupitia Global T V Online ambayo itarusha mubashara kabisa kutokea ndani ya ukumbi.
“Tumeamua kufanya hivi ili kuwapunguzia shida watu kutoka sehemu mbalim bali kufika ukumbini ili kuweza kuona moja kwa moja na badala yake wataweza kuangalia kila k i n achotokea ukumbini kupitia katika simu zao za mkononi.
“Sisi kama TBPO tumeomba udhamini wa Global TV na wamekubali, ni kitu cha kupongezwa, tunamshukuru sana Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo kwa kukubali kwake pambano hili lirushwe moja kwa moja ili watu wengi waweze kujionea kwa urahisi kabisa maana wao ndiyo wamegharamikia kila kitu.
“Sasa kuweza kushuhudia mapambano hayo katika simu tena bure basi hakikisha unajiunga (subscribe) na YouTube Channel ya Global TV Online.
“Unachotakiwa kufanya ni kuingia YouTube, tafuta Global TV Online, kisha ubonyeze neno SUBSCRIBE, pia ubonyeze kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.
“Lakini kama umeshajiunga, basi hakikisha umebonyeza hicho kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea ndani ya Global TV. Nje ya hapo unaweza kuipata kupitia mtandao wao wa www. globaltvtz.com.
“Niwaombe mabondia wetu kuwa fursa hii ya kuweza kupata pambano hili ambalo litarushwa moja kwa moja ni kitu kikubwa sana kwao maana itasaidia kuweza kuwauza sokoni kirahisi.
“Kila mtu atakuwa amewaona wakati wa wakicheza bila ya kusimuliwa, nasema hivi kutokana na tayari nimeshaanza kupokea simu kutoka katika baadhi ya mataifa ya Ulaya kuhusu hili pambano.
“Nataka mabondia wetu wacheze vizuri, sina wasiwasi na mabondia wanaokuja, ni wakali na wanarekodi nzuri lakini nataka mabondia wetu wacheze na wapigane kwelikweli,” anasema Ustaadh.
Katika hatua nyingine, pambano hilo, halitakuwa na kiingilio na mashabiki wataweza kulishuhudia mubashara kupitia simu zao za mkononi tu, kwani litaonyeshwa na Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko tu.